Nchi ya Burundi
imeishutumu Rwanda kwa madai ya kupanga kufanya majaribio ya kutaka kumuua
msaidizi wa Rais Pierre Nkurunziza, Willy Nyamitwe.
KUHABARISHA NA KUFAHAMISHA KUHUSU HABARI NA MAMBO YANAYOENDELEA KATIKA JAMII YA GEITA, KANDA YA ZIWA, TAIFA NA DUNIANI. TUTUMIE HABARI AU WASILIANA NASI KUPITIA info@stormfm.co.tz au +255 685 883 870
Wednesday 30 November 2016
Tuesday 29 November 2016
WIZARA YA ELIMU YAKANUSHA TAARIFA ZINAZOSAMBAA KUWA WANAFUNZI WA DIPLOMA KUTOJIUNGA NA VYUO VIKUU
Wizara ya Elimu,
Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi imetoa ufafanuzi kwamba haijapiga
marufuku watu wenye Stashahada wenye sifa kujiunga na vyuo vikuu badala yake
walichokataza ni wanafunzi waliofeli kidato cha nne na cha sita kujiunga na
vyuo vikuu bila kuwa na vyeti vyenye sifa.
PICHA:WAZIRI NAPE KATIKA MAKABIDHIANO YA PICHA YA RAIS
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati)
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kabla ya makabidhiano ya
picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli iliyochorwa
na kikundi cha Angavu Youth Group jijini
Dar es Salaam. Picha hiyo imekabidhiwa kwa Waziri huyo kwa niaba ya Mhe. Rais. kushoto ni Mwenyekiti
wa Angavu Youth Group Bw. Athumani Salum na kulia ni Katibu wake Bi. Oliver
Charles.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (kulia) akisikiliza kwa makini hotuba
iliyokuwa ikisomwa na Katibu wa Angavu Youth Group Bi.Oliver Charles (katikati)
wakati wa makabidhiano ya picha ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli jijini Dar es
Salaam.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (kulia) akipokea
picha ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutoka
kwa Mwenyekiti wa Angavu Youth Group Athumani Salum (kulia) jijjini Dar es Salaam. Picha hiyo imechorwa
kwa ustadi na kikundi cha Angavu Youth Group.
Muonekano
wa picha ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli iliyoichora kwa ustadi na
kikundi cha Angavu Youth Group ambapo imekabidhiwa jijini Dar es Salaam kwa Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye kwa niaba ya Mheshimiwa
Rais.
RAIS DKT.MAGUFULI AMWANDALIA RAIS EDGAR LUNGU DHIFA YA KITAIFA IKULU JIJINI DSM
Sunday 27 November 2016
AMIRI JESHI MKUU RAIS DKT MAGUFULI ATUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WANAFUNZI KUNDI LA 59/15 IKULU JIJINI DSM
Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitunuku kamisheni kwa Maafisa
Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika
viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 2016
Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akikagua gwaride la heshima
linaloundwa na Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la
Tanzania (JWTZ) kabla hajawatunuku kamisheni katika viwanja vya Ikulu jijini
Dar es salaam Novemba 26, 201
Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini kwenye hati ya
kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la
Tanzania (JWTZ) kabla hajawatunuku katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es
salaam Novemba 26, 201
Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea baada ya kutunuku kamisheni
kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ)
katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 201
Subscribe to:
Posts (Atom)