Thursday 21 December 2017

JESHI LA POLISI LIMESEMA MAKOSA YA JINAI YAMEPUNGUA NCHINI


Jeshi la Polisi nchini limetamba kushinda vita dhidi ya uhalifu baada ya kupunguza matukio ya aina hiyo huku likikiri kuongezeka kwa vitendo vya ubakaji na kunajisi.

Tuesday 19 December 2017

DAKTARI FEKI ANASWA HOSPITALI YA MKOA WA MWANZA


Jeshi la polisi mkoani Mwanza linamshikilia mtu mmoja kwa kosa la kujifanya daktari, katika hospitali ya mkoa Sekou Toure.

TAARIFA YA CHADEMA JUU YA UTEUZI WA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SINGIDA KASKAZINI


Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) amesikika asubuhi hii wakati akihojiwa na Radio Clouds Fm kwenye kipindi cha Power Breakfast, akisema kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimechukua fomu za kugombea ubunge katika uchaguzi wa marudio Jimbo la Singida Mashariki, mkoani Singida.

Kupitia taarifa hii ya awali, tungependa vyombo vya habari na umma kwa ujumla ujue kuwa;

1. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hakijateua mgombea kuwania nafasi ya ubunge katika uchaguzi huo wa marudio, Jimbo la Singida Kaskazini.

2. Mkurugenzi wa NEC, Ndugu Ramadhan Kailima atambue kuwa suala la kugombea nafasi ya ubunge kwa mchakato wa ndani ya CHADEMA linasimamiwa na Kamati Kuu ya Chama na hivyo hivyo yeye hana mamlaka wala hawezi kuwa msemaji wa suala hilo katika hatua ya sasa.

3. Tunafuatilia kupata taarifa za kina kuhusu msingi wa kauli ya Mkurugenzi hiyo, kisha tutatoa taarifa kamili katika hatua ya baadae.

Imetolewa leo Jumanne, Desemba 19, 2017 na;

Tumaini Makene
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano

Monday 18 December 2017

VODACOM TANZANIA FOUNDATION, DORIS MOLLEL FOUNDATION WATOA MSAADA WA VIFAA TIBA VYENYE THAMANI YA SH ,MILIONI 24 KWENYE HOSPITALI YA WILAYA YA CHATO, GEITA

DSC_1104
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya akipokea moja ya mashine za kusaidia kupumua watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti) kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (kushoto) kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Chato, Mkoani Geita. Msaada huo umetolewa kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Vodacom Tanzania pamoja na Taasisi ya Doris Mollel. Wanaoshuhudia ni Muasisi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njini nchini, Doris Mollel (wa pili kushoto) na Kushoto ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Chato, Dkt. Ligobert Kalasa.

DSC_1092
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa msaada wa vifaa tiba kwa ajili ya kusadia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati kwa Hospitali ya Wilaya ya Chato Mkoani Geita, uliotolewa kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Vodacom Tanzania (Vodacom Tanzania Foundation) pamoja na Taasisi ya Doris Mollel (Doris Mollel Foundation). hafla hiyo imefanyika leo katika Hospitali ya Chato, Mkoani Geita.

DSC_1095
Baadhi ya vifaa tiba ambavyo vimetolewa kwenye hospitali ya Wilaya ya Chato Mkoani Geita ambavyo vitaweza kuwasaidia watoto ambao wanakuwa bado hawajafikia muda wa kuzaliwa.

DSC_1107
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya akimkabidhi vifaa na  mashine za kusaidia kupumua watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (Njiti) katibu tawala wa Wilaya ya Chato kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya hiyo, Mkoani Geita. Msaada huo umetolewa kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Vodacom Tanzania pamoja na Taasisi ya Doris Mollel. 

DSC_1115
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Chato,Dkt. Ligobert Kalasa akitoa maelezo ya namna ambavyo mashine hizo zinatumika.

DSC_1117
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya akiteta jambo na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia pamoja na Muasisi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njini nchini, Doris Mollel.

DSC_1131
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya akiteta jambo na Mganga mfawidhi wa hospital ya wilaya ya Chato Ligobert Kalasa wakati alipokuwa akielekea kwenye wodi za watoto ambao wamezaliwa kabla ya wakati.
DSC_1135
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya akitoa maelezo juu ya kitanda cha wagonjwa ambacho kilikuwa nje ya hospital.



DSC_1181
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya akimkabidhi zawadi ya Khanga Bi.Lucia  Jamesi pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia  aliyekuwa katika Wadi ya Wazazi ya Hospitalini hapo.

DSC_1211
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia akimsalimia mmoja wa watoto waliozaliwa katika Hospitali ya Chato, Mkoani Geita leo.

DSC_1222
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (katikati) pamoja na Muasisi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njini nchini, Doris Mollel wakipanda mti katika eneo la Hospitali ya Chato ikiwa ni ishara ya mtoto anayezaliwa na kutunzwa katika mazingira bora.

DSC_1245
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (katikati) pamoja na Muasisi wa Taasisi ya Doris Mollel na Balozi wa Watoto Njini nchini, Doris Mollel  wakiwamwagia maji mti ambao wameupanda.

KINANA ASEMA YUPO TAYARI KUITUMIKIA CCM....ATOBOA SIRI YA USHINDI WA KISHINDO


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amesema yuko tayari kuendelea kukitumikia chama hicho.

Neno la mwenyekiti kwangu ni amri kama umeona bado unahitaji niendelee kukusaidia niko tayari kufanya hivyo,” alisema Kinana leo Jumatatu Desemba 18,2017 katika mkutano mkuu wa CCM unaoendelea mjini Dodoma.

Kinana ametoa kauli hiyo wakati kukiwa na minong’ono kuwa ameandika barua akiomba kuachia nafasi yake ya ukatibu mkuu.

Awali, Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli aliweka wazi kuwa Kinana amekuwa msaada mkubwa katika kukiongoza chama hicho.

“Mzee Kinana amenisaidia sana. Amenisaidia mno kwenye kufanya mabadiliko ndani ya chama na ni mategemeo yangu ataendelea kunisaidia,” alisema.

Katika hatua nyingine, Kinana ametoa siri ya ushindi wa kishindo wa chama hicho katika uchaguzi kuwa ni kutokana na ilani bora, demokrasia  na kusikilia maoni ya wanachama.

Kinana amesema demokrasia imekuwa msingi wa chama hicho ndiyo sababu kinaimarika.

“CCM tunazingatia demokrasia, wanachama wapo huru kutoa maoni ndani ya chama. Hili linafanyika kwa kuwa usipowapa uhuru wa kusema ndani watasema nje,” alisema.

SERIKALI MKOANI GEITA YAJIPANGA KUTATUA TATIZO LA MAJI KWA WANANCHI

DSC_0761
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Gabriel akiwa na Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Geita(GEUWASA)Mhandisi Joseph Mwita wakati alipotembelea moja kati ya mitambo ya kuzalishia maji ambayo hipo kijiji cha Nungwe kwenye ziwa viktoria.

DSC_0754
Eneo la mitambo ya uzalishaji wa maji ambayo hipo kijiji cha Nungwe.

DSC_0814
Fundi  wa mitambo ya maji kutoka mgodi wa dhahabu wa Geita,(GGM)Denis Domician akitoa maelezi namna ambavyo maji yamekuwa yakitibiwa kabla ya kusambazwa kwa watumiaji mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Geita.

DSC_0837
Fundi  wa mitambo ya maji kutoka mgodi wa dhahabu wa Geita,(GGM)Denis Domician  akitoa maelezo namna ambavyo maji yamekuwa yakipita na kutibiwa kwenye sehemu ambazo zimetengwa.

DSC_0846
Eneo la kutibia maji.

DSC_0862
Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshugulikia masuala ya Bonde la Ziwa Victoria Dr Ali Said Matano akielezea namna ambavyo jumuiya hiyo imeweza kuongeza muda kwa miradi ambayo ijamalizika hadi kufikia mwezi wa tisa mwakanai iwe imekamilika wakati wa ziara ya kutembelea vyanzo vya maji ambavyo vipo kwenye halmashauri ya mji wa Geita. 

DSC_0881
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Gabriel pamoja mhandisi wa maji wa Geuwasa wakitoa maelezo ya namna ambavyo Tanki hilo limekuwa kikifanya kazi wakati alipotembelea kwenye tanki hilo.

DSC_0890
Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinal akitoa maelezo ya namna ambavyo wanatarajia kupitisha mabomba kwenye mtaa wa 14 kambarage kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita.

Friday 15 December 2017

SPIKA WA BUNGE AAHIDI KWENDA NAIROBI KUMTEMBELEA TUNDU LISSU


Spika wa Bunge, Mhe.  Job Ndugai amefunguka na kusema atakwenda jijini Nairobi nchini Kenya kumuona Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambaye anafanyiwa matibabu katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya kufuatia kupigwa risasi Septemba 7, 2017.

WANAWAKE WALIOVISHANA PETE WAACHIWA KWA DHAMANA


Washtakiwa wanne katika shauri la kufanya vitendo vinavyoashiria mapenzi ya jinsia moja na makosa la kimtandao wameachiwa kwa dhamana baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza kutupilia mbali hoja za kuzuia dhamana zao zilizowasilishwa na upande wa Jamhuri.

Wednesday 6 December 2017

NAIBU WAZIRI MAZINGIRA ASWEKA NDANI VIGOGO WATANO MKOANI GEITA KUTOKANA NA UKIUKWAJI WA SHERIA ZA MAZINGIRA

DSC_0677
Naibu Waziri wa Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais Inayoshughulika na muungano na Mazingira Mheshimiwa Kangi Lugola akizungumza na wananchi ambao mashamba yao yameathirika kutoka na sumu ambayo imeeharibu mazao yao pamoja na viumbe hai.
DSC_0575
Moja kati ya wakurugenzi wa Mgodi wa  Nyarugusu Mine Co.Limited  Fred Masanja akionesha cheti NEMC ambacho naibu waziri alikikata.

DSC_0594
Bwawa la kuhifadhia maji ya kemikali ambalo limeharibika na kusababisha maji mengi kuelekea kwenye shughuli za wananchi.

DSC_0597
Naibu Waziri wa Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais Inayoshughulika na muungano na Mazingira Mheshimiwa Kangi Lugola ,akiwa na mwenyeji wake ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Geita wakikagua eneo ambalo lilipasuka na kupeleka maji ya sumu kwenye maeneo ya mashamba ya wananchi.

DSC_0598
Naibu Waziri wa Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais Inayoshughulika na muungano na Mazingira Mheshimiwa Kangi Lugola  akiangalia baadhi eneo ambalo limepasuka.

DSC_0663
Naibu Waziri wa Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais Inayoshughulika na muungano na Mazingira Mheshimiwa Kangi Lugola  ,akitembelea na kuangalia miche ya miti ambayo imekwisha kuathirika.

DSC_0667
]Naibu Waziri wa Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais Inayoshughulika na muungano na Mazingira Mheshimiwa Kangi Lugola ,akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi na baadhi ya wananchi ambao wameathirika kutokana na maji Hayo kwenye maeneo ya mashamba.

Tuesday 5 December 2017

MGODI WA DHAHABU WA GGM MABINGWA MICHEZO YA SHIMMUTA



Mgodi wa Dhahabu Geita (GGM) umeibuka kidedea kwenye Mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma na Makampuni binafsi Tanzania (SHIMMUTA) yaliyomalizika Disemba Mosi kwenye Viwanja vya Samora Mjini Iringa