Ajali ya moto imetokea
katika mtaa wa Balenge kata ya Kalangalala katika nyumba ya kulala wageni majira
ya leo mchana wilayani na mkoani Geita na kusababisha uharibifu wa vitu vya
thamani baada ya nyumba kuungua moto.
Wakizungumza na storm
habari wakazi wa eneo hilo ambao wamejitokeza eneo la tukio kushuhudia huku
wakisaidia zoezi la uokoaji wamesema kuwa moto huo ulianzia katika chumba baada
ya mtumiaji wa chumba hicho kuacha jagi la kuchemshia maji likiwa halijazimwa kwenye umeme.
Akizungumza katika eneo
la tukio kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Geita Inspector Christina Sunga amewataka wananchi wa mkoani hapa
kwa ujumla kuwasiliana na jeshi hilo haraka pindi zinapotokea ajali kama
hizo kwa kupiga simu moja kwa moja jeshi la zimamoto ili kupatiwa msaada.
Kwa upande wake Evarist
Mwanakatwe ambaye ni Afisa wa kitengo cha dharula katika mgodi wa dhahabu wa
Geita (GGM) baada ya kufika katika eneo la tukio wakiwa na gari la zimamoto na
kuwezesha zoezi la uokoaji kumalizika katika hali ya usalama amewapongeza
wakazi wa mtaa wa Balenge kwa kuchukua uamuzi wa kutoa msaada wa uokoaji.
Naye mtoto wa mmiliki
wa nyumba hiyo Bainika Kwitega Balenge ameshukuru wananchi pamoja na jeshi la zimamoto
wakisaidiana na mgodi wa GGM kwa
kuwezesha uokoaji wa
nyumba hiyo.
No comments:
Post a Comment