Katika mazungumzo ya viongozi wa nchi hizo mbili, Rais
Uhuru Kenyatta wa Kenya ameeleza kufurahishwa kuona Rais John Magufuli wa
Tanzania yupo tayari kuhakikisha nchi hizo zinakuwa karibu na miradi ya
maendeleo inaharakishwa.
Mradi mwingine wa maendeleo walio ujadili ni kuzalisha
ajira kupitia viwanda.
'' Kwa sababu nia yetu sisi ni kuona maendeleo
yatakayogusa wananchi wa kawaida, tumalize umasikini, uchumi ukue, na hivyo
hatuwezi kufanya tukiwa tumetengana'' alisema Kenyatta.
Kwa upande wake Rais Magufuli amesema Tanzania na Kenya
zina kila sababu za kuimarisha mahusiano ya kibiashara hasa katika ujenzi wa
viwanda, utakaozalisha ajira kwa kuwa watu wake ni wamoja.
''Wazee
wetu mzee Kenyatta na mzee Nyerere walijenga mazingira mazuri ya kuwa na nchi
hizi mbili, wakati wakipigania uhuru, sasa sisi vijana wetu ni wakati wetu
kwenda mbele kwa ajili ya maendeleo''
alisema Rais Magufuli.
Rais Magifuli ameutaja mradi moja wapo kuwa ni ujenzi wa
njia ya kusafirisha umeme kutoka Tanzania kwenda Kenya kupitia Namanga.
No comments:
Post a Comment