Balozi Ambeyi Ligabo akifuatiwa na Mwenyekiti wa Mkutano, Service Julie kutoka Congo.
|
Wataalam wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR wakiendelea na majadiliano
|
Wataalam wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR wakiendelea na majadiliano Jijini Arusha.
|
Wataalam wa Madini ya Dhahabu kutoka Nchi za Ukanda wa
Maziwa Makuu ICGLR wamekutana Jijini Arusha ili kujadili masuala mbalimbali
yanayohusu madini hayo kwa maslahi mapana ya nchi hizo.
Mkutano huo wa siku mbili ulifunguliwa jana Machi 27,
2018 na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ambapo alisisitiza kuwa Nchi
Wanachama wa ICGLR wanao wajibu wa pamoja kuhakikisha malengo waliyojiwekea
yanafikiwa kwa manufaa ya wanachama wote.
Gambo alizungumzia changamoto mbalimbali
zinazozikabili Nchi Wanachama ambazo ni uvunaji haramu wa madini, utoroshwaji
wa madini, uharibifu wa mazingira, ukosefu wa teknolojia na baadhi ya Nchi kuwa
na changamoto za Kiusalama.
Hata hivyo alisema changamoto hizo zisiwe sababu ya
kurudi nyuma badala yake juhudi za pamoja, mshikamano wa dhati unahitajika ili
kukabiliana na changamoto hizo na kuhakikisha ufumbuzi unapatikana kwa maslahi
mapana ya Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu.
Nchi Wanachama ni Tanzania, Angola, Burundi, Jamhuri
ya Afrika ya Kati, Congo (Kinshasa), Congo (Brazzaville), Kenya, Rwanda, Sudan
Kusini, Sudan Kaskazini, Uganda na Zambia.
Tanzania imekuwa Mwanachama rasmi wa ICGLR Mwaka 2008
na tangu wakati huo imeendelea kutekeleza malengo ya mpango wa ICGLR ili
kufanikisha udhibiti wa uvunaji haramu wa madini na kuhakikisha manufaa ya
pamoja ya rasilimali husika yanapatikana.
No comments:
Post a Comment