Wananchi wa Zanzibar
leo wanapiga kura katika uchanguzi wa marudio baada ya kufutwa kwa uchanguzi
uliofanyika October 25,2015 kutokana na kasoro zilizojitokeza.
Katika baadhi ya vituo wananchi wamejitokeza na zoezi linaendelea vizuri huku
hali ya usalama ikiwa imeimarishwa.
Katika kituo cha shule
ya sekondari Muembeladu ambayo ina vituo sita,vituo vitano vinawatu 350 na
kituo kimoja kina watu 91. Akizungumza na wanahabari, msimamizi wa kituo hicho
amesema zoezi la upigaji kura linaendelea vizuri katika jimbo la Jangombe .
Kwa upande wa kituo
cha skuli ya Muembeshauri nako hali ni shwari na zoezi linaendelea vizuri
ambapo katika skul hiyo vituo 11 vinatumika watu kupiga kura.
Katika Jimbo la
kikwajuni, zoezi linaendelea vizuri huku mwitikio wa watu ukiwa ni
mkubwa.
Baadhi ya wananchi
waliojitokeza kupiga kura wamesema zoezi hilo limekua rahisi na la amani
tofauti na taarifa zilivyokua zinasambazwa.
Mkazi wa Muembeshauri
aliyejitambulisha kwa jina la Hamidu Salum Haji ametoa wito kwa wananchi
kujitokeza kwa wingi kwani zoezi la kupiga kura linaendelea kwa amani na
utulivu.
“Ndugu zangu tusikubali kugombanishwa na watu
ambao hawaitakii mema Zanzibar tusimame pamoja katika kutetea nchi yetu” amesema Haji
Wakati zoezi hilo
linaendelea maduka mengi yamefunguliwa na wafanyabiashara wanaendelea na kazi
kama kawaida.
No comments:
Post a Comment