Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na Manase Mjema, Diwani wa Kimanga wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo asubuhi na kusomewa shitaka la kudhuru mwili ambapo wote wawili wamekana shitaka hilo.
Watuhumiwa hao
wanatuhumiwa kumshambulia Terresia Mmbaando, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar
es Salaam wakati wa mkutano wa uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es
Salaam tarehe 27 Februari 2016.
Kubenea anatajwa kuwa
ni mtuhumiwa namba sita ambapo Manase akiwa mtuhumiwa namba nne.
Mmbando alikuwa
mwenyekiti wa mkutano wa kumchagua Meya wa Jiji la Dar es Salaam uliofanyika
kwenye Ukumbu wa Kareem Jee na baadaye kuahirishwa hatua ambayo iliibua
malumbano.
Mbele ya Cyprian
Mheka, Hakimi Mkazi Kisutu washitakiwa hao walikana kosa hilo ambapo hakimu
alighairisha kesi hiyo mpaka tarehe 16 Machi mwaka huu.
Hata hivyo, Hakimu
Mkeha aliwataka watuhumiwa hao kujidhamini wenyewe kwa dhamana ya Sh. 2,000,000
sharti ambalo wamelitekeleza.
Jana asubuhi kwenye
mahakama hiyo Kubenea akihudhuria kesi yake dhidi ya Paul Makonda, Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni, alikamatwa na Jeshi la Polisi na kuwekwa chini ya ulinzi.
Kubenea na Manase
wameunganishwa kwenye kesi hiyo ambapo watuhumiwa waliofikishwa mahakamni
awali ni Halima Mdee, Mbunge wa Kawe; Mwita Waitara, Mbunge wa Ukonga na
madiwani wawili jumla yao ikiwa ni watuhumiwa sita.
No comments:
Post a Comment