Rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli
amewasihi watanzania kuendelea kuwa wamoja na kushirikiana kuijenga nchi yao badala
ya kubaguana.
Ametoa wito huo katika
kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Azania front jijini
Dar es salaam, aliposali ibada ya pasaka pamoja na waumini wa kanisa
hilo.
Amesema mwenyezi mungu
alimtoa mwanae wapekee yesu kristo kuja kuikomboa dunia bila kuwabagua
wanadamu, vivyo hivyo nasi binadamu wanapaswa kutobaguana, iwe kwa dini,
makabila, mitazamo ya kisiasa na hata rangi
zetu.
Aidha Rais Magufuli amewakumbusha watanzania
kufanya kazi kama ambavyo vitabu vitakatifu vinasisitiza umuhimu wa kufanya
kazi, na amebainisha kuwa tanzania yenye neema inawezekana endapo kila mtu
atazingatia kufanya kazi.
Katika hatua nyingine
pia amewaomba watanzania kuendelea kuliombea taifa lao na pia kumuombea yeye
ili afanikiwe kutekeleza jukumu kubwa na zito la kuiongoza nchi pamoja na kuongoza maombi ya kumuombea
Raisi Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli waliohudhuria ibada hiyo, Askofu
mkuu wa KKKT Dayosisi ya mashariki na pwani Dkt.Alex Malasusa amempongeza Raisi
magufuli kwa tabia yake ya kupenda kuhudhuria ibada na
kuwasihi viongozi wengine kupenda ibada.
Askofu Malasusa
ameuelezea ufufuo wa yesu kristo kuwa jambo la kuleta matumaini,na hivyo
amepongeza mwelekeo wa nchi kwa sasa huku akisema kanisa linaona matumaini kwa taifa.
No comments:
Post a Comment