Serikali Mkoani Mwanza
inatakiwa kuboresha vifaa vya ulinzi na usalama katika visiwa vilivyo
ndani ya ziwa Victoria ili kuweza kuinua huduma za uokozi na usalama wa raia
mali zao visiwani humo.
Akikabidhi Ofisi ya Mkoa
kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza Mpya John Mongera Mkuu wa mkoa wa zamani Magessa
Mulongo amesema kuwa mkoa uko salama lakini kuna uhaba wa vifaa vya ulinzi na
usalama hasa vya majini.
Bw. Mulongo amesema kuwa
kuna uhitaji wa Boti za mwendo kasi kwa ajili ya vikosi vya usalama ili kuweza
kufika maeneo ya matukio kwa haraka katika visiwa vilivyo ndani ya ziwa
Victoria ikiwemo ukerewe na Ilugwa, hali itakayo saidia kudhibiti uhalifu
mkoani humo.
Aidha Mkuu wa mkoa mpya
Bw.John Mongera akipokea taarifa ya makabidhiano ya mkoa ameshukuru na
kuahidi kuendeleza mazuri yaliyofanywa na mtangulizi wake ikiwa ni pamoja na
kudumisha amani na salama wa mkoa huo.
Makabidhiano hayo
yamefanyika baada ya Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe
magufuli kufanya uteuzi mpya wa wakuu wa mikoa, huku Mulongo amehamishiwa mkoa
wa Mara na nafasi yake kuchukuiwa na Mongera akitokea Mkoa wa Kagera.
No comments:
Post a Comment