Kufuatia agizo la
serikali la kutoa elimu bure kuanzia ngazi ya msingi hadi kidato cha 4,
baadhi ya shule za msingi mkoani hapa ikiwemo
Lutozo ,Ludete, na Nyawilimilwa zimeonekana kuandikisha idadi kubwa ya
wanafunzi huku shule hizo zikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo
upungufu wa walimu, madawati, na vyumba
vya madarasa hali ambayo inapelekea wanafunzi kusoma wakiwa chini ya mti na
wakati mwingine hulazimika kurudi nyumbani pindi mvua zinaponyesha kutokana na
kukosa mahali pa kujikinga.
Wakizungumza na Storm
habari walimu wakuu wa shule hizo Lukas
Mabula wa Ludete, Hoza Mayunga, wa Nyawilimilwa,na Masota Elioza wa Lutozo,
wamesema kuwa changamoto hizo zimekuwa zikiwafanya kushindwa kuifanya
kazi yao kiufanisi na kwamba wameiomba serikali na wadau mbalimbali wa elimu
kusaidia kuboresha miundo mbinu mashuleni ili kuendelea kukuza taaluma nchini.
Storm habari
imefika katika shule hizo na kujionea namna wanafunzi hao wanavyokumbana
na changamoto hizoikwemo kukaa chini huku
wakiyoomba serikali kuboresha miundo mbinu katika shule zao ili waweze kusoma
vizuri na baadae kupata wasomi wengi
watakao saidia kuleta maendeleo nchini.
Hata hivyo afisa
elimu wa shule za msingi wilayani Geita bw, Deusi Sefu amekiri kuwepo kwa
changamoto katika shule hizo na kwamba amesema serikali imeeanza kuchukua hatua
juu ya jambo hilo ambapo imetenga milioni 303 kwa ajili ya kutengeza madawati
ikiwa ni pamoja na kusitisha baadhi ya miradi ya mendeleo iliyokuwa ikiendelea
wilayani hapa ili kupisha uboreshaji wa miundo mbinu mashuleni.
Aidha afisa elimu Sefu
amewaomba wadau na mashirika mbalimbali nchini kujitokeza kuchangia
mashuleni ili kuendelea kuboresha
taaluma nchini.
No comments:
Post a Comment