Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya udhibiti wa huduma ya nishati na maji(EWURA), Felix Ngamlagosi.
Bei ya nishati ya mafuta imeendelea kushuka baada ya mamlaka ya
udhibiti wa huduma za nishati na maji Ewura kutangaza bei kikomo.
Akitangaza bei elekezi ya mafuta hayo jijini dar es salaam itakayoanza
kutumika nchini kuanzia leo tarehe 02 march mkurugenzi mkuu wa
mamlaka ya udhitibiti wa nishati na maji (EWURA) Bw.Felix Ngamlagosi
amesema bei ya petroli imeshuka kwa sh. 31, dizeli sh 114 na mafuta ya taa
yameshuka kwa sh, 234.
Amewataka wateja wa nishati ya mafuta kudai risiti pindi
wanapopewa huduma hiyo na kwamba kuanzia sasa wananchi wanaweza kupata bei hizo
kupitia simu zao za kiganjani.
Aidha ameongeza kuwa
hakutakuwa na mabadiliko ya bei ya mafuta ya petroli na dizeli kwa mkoa wa tanga
kwa mwezi marchi kutokana na kutopokelewa kwa mafuta mapya kupitia bandari ya
tanga mwezi februari mwaka huu.
No comments:
Post a Comment