1. Mkuu wa Hifadhi ya Saadani Bw.
Hassan Nguluma akiwaonesha Wajumbe wa Kamati ya Maliasili, Utalii na Ardhi
ramani ya Hifadhi hiyo wakati kamati hiyo ilipoitembelea Hifadhi ya Saadani
pamoja na kukutana na Menejimenti ya TANAPA. Wengine katika picha ni Naibu
Waziri wa Utalii na Maliasili Mhandisi Ramo Makani (mweye miwani) na Kulia
kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe Atashasta Nditiye.
2. Mwenyekiti
wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe Atashasta Nditiye akizungumza na Menejimenti
ya TANAPA wakati kamati hiyo iliopotembelea Hifadhi ya Saadani. Kulia kwake ni Naibu
Waziri wa Utalii na Maliasili Mhandisi Ramo Makani
3. Mkurugenzi wa Masoko na Utalii wa TANAPA Bw. Ibrahim Musa akitoa
ufafanuzi wa masuala mbalimbali wakati akizungumza na Wajumbe wa Kamati
ya Ardhi, Maliasili na Utalii. Kamati hiyo ilikutana na TANAPA katika Hifadhi
ya Saadani.
4. Naibu
Waziri wa Utalii na Maliasili Mhandisi Ramo Makani akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii. Kamati
hiyo ilikutana na TANAPA katika Hifadhi ya Saadani.