Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mwigulu Lameck Nchemba, ametolea ufafanuzi suala
lililoibuliwa na Mbunge wa Kilwa Kusini Suleiman Bungara, kuhusu polisi
kushambulia watu msikitini na wengine kuuawa.
Akizungumza
Bungeni leo Waziri Nchemba amesema kwamba yeye kama waziri mwenye dhamana
amelisikia suala hilo na ameagiza uchunguzi ufanyike, ili kuweza kubaini mbivu
na mbichi na sheria kufuata mkondo wake.
Sambamba na hilo Waziri Nchemba ameitaka jamii
kutohusisha makosa ya uhalifu na masuala ya dini au siasa, kwani mhalifu
anapokamatwa hakamatwi kwa imani ya dini au chama chake, bali ni kwa makosa
aliyofanya.
“Nimewaelekeza wafanye uchunguzi wa ndani ili tuweze
kupata taarifa kamili na tutatoa taarifa, na nimuombe mheshimiwa mbunge tuepuke
sana kulinganisha jambo hilo na dini, linapotokea suala la uhalifu mtu
hakamatwi kwa dini yake, anakamatwa kwa kosa alilolifanya, watu wanakamatwa
kutokana na makosa aliyofanya wala asiunganishwe kwa dini yake au chama chake”, amesema Mwigulu Nchemba.
Hapo jana Mbunge wa kIlwa Kusini Suleiman
Bungara maarufu kwa jina la Bwege alimtaka Waziri atolee ufafanuzi suala la
polisi kuingia msikitini na kupiga risasi, na kuchukua baadhi ya watu ambao
wengine walirudi wakiwa marehemu.
No comments:
Post a Comment