Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Msukuma amesema kufungia nyimbo za wasanii Nchini si jambo sahihi kwa Maendeleo ya Wasanii hao.
Akizungumza katika
mjadala wa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Mwaka
2018/19, Msukuma amesema Wasanii nchini wanalenga Soko la kimataifa na kwamba
haiwezekani wapeleke Video za nyimbo zao katika soko la kimataifa ikiwamo
Marekani wakiwa wamerekodi huku wamevaa Madela.
Amesema ni jambo
lisiloingia akilini watu kutazama video za mwanamuziki Rihanna katika vituo
mbalimbali vya televisheni, huku wahusika wakiwa wamevaa nusu utupu, huku zile
za Tanzania zikifungiwa.
“Mtu kaimba wimbo
mwaka mzima uliopita leo waziri unaibuka na kufungia. Huko vijijini watu
wameshaipata hizo nyimbo, mnatupa taabu sana huko vijijini maana watendaji
wanakamata kompyuta za watu zenye nyimbo zilizofungiwa,” amesema Msukuma.
“Msitumie muda mwingi
kufungia nyimbo, tumieni muda mwingi kuwaelimisha hawa wasanii maana wanatumia
muda mrefu sana kutengeneza nyimbo zao.” Alimalizia kwa kusema hivyo
No comments:
Post a Comment