Serikali Mkoani Geita
imewaonya watu au vikundi ambavyo vitaonekana kuvunja amani ya Mkoa na
kwamba mkoa upo imara katika kudumisha suala la ulinzi na usalama.
Hayo yamesemwa na Mkuu
wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Gabriel wakati alipokuwa akizungumza na vikosi
vya ulinzi na usalama nje ya ofisi za mkoa.
Amesema ni vyema kwa
jamii ikatambua kuna walinzi hivyo wanawajibu wa kutii sheria
bila ya kushuru kwenye maeneo ambayo wanaishi.
Aidha Mkuu wa mkoa
Ameongeza kwa kusema anatambua changamoto walizonazo Askari katika utendaji wao
wakazi hivyo ilikuwafanya wapate nguvu za kufanya kazi tayari wamekwisha kuanza
mchakato wa ujenzi wa Nyumba 100.
Mkuu wa Mkoa amesema
kumekua na imani potofu za mauaji ya vikongwe, Maaskari na walinzi kwa
imani ya kupata mali kupiti damu ya watu hao,hivyo ameagiza vikosi hivyo
kupinga na kupambana vikali na vitaa hiyo ili kutokomeza mauwaji hayo.
Mkoa wa Geita Upo
kwenye Kampeni ya Wiki mbili ambayo inaitwa TAFAKARI YA ULINZI NA USALAMA MKOA
WA GEITAinayotarajia kumalizika tarehe 28 ambayo inalengo la kudumisha
amani ya Mkoa huo.
No comments:
Post a Comment