Rais Kim Jong-Un wa
Korea Kaskazini amekuwa kiongozi wa kwanza wa taifa hilo kuvuka mpaka wa
kijeshi uliowekwa kuzitenganisha nchi hizo mbili baada ya vita ya mataifa hayo
mawili mwaka 1953. Akiwa ni mwenye tabasamu rais Korea kusini Moon Jae-in
amempokea mgeni wake katika eneo la mpakani.
Ni miaka 65 hadi sasa
kwa kiongozi wa Korea Kaskazini kuwahi kuvuka mpaka wa kijeshi uliowekwa
kuzitenganisha Korea Kaskazini na Korea Kusini tangu kumalizika kwa vita vya
mataifa hayo mawili mwaka 1953.
Eneo la mpaka huo
aliouvuka Kim Jong Un wakati akielekea Korea kusini ni lenye kilomita 250 na
upana wa kilomita nne,ambapo mara baada ya kuuvuka tu watu walipiga makofi kwa
kuandikwa kwa historia.
Mkutano huo wa tatu
baada ya mkutano wa mwaka 2000 na 2007 ni matokeo ya jitihada zilizofanyika
miezi kadhaa kuimarisha mahusiano kati ya Korea hizi mbili na kufungua milango
ya mkutano kati ya Kim na Rais wa Marekani Donald Trump.
Kim alitangaza juma
lililopita kuwa angesitisha zoezi la majaribio ya silaha za nuklia kwa
sasa.Hatua hiyo ilikaribishwa na Marekani na Korea Kusini kama hatua
nzuri,ingawa watafiti wa China wameonyesha kuwa eneo linakofanyika jaribio la
nuklia la Korea Kaskazini huenda lisitumike tena baada ya mwamba kuporomoka
baada ya jaribio la mwisho la mwezi Septemba.
Korea Kusini na
Marekani zimesema zinasitisha mazoezi ya kijeshi kwa siku moja kupisha mkutano
huo.
Kim ameongozana na
maafisa tisa, akiwemo dada yake, Kim Yo-jong,aliyeongoza ujumbe wa Korea
Kaskazini kwenye michuano ya Olimpiki nchini Korea Kusini mapema mwaka
huu.Mkutano huu pia utawahusisha maafisa wa juu wa kijeshi na wanadiplomasia.
No comments:
Post a Comment