Katika hali hisiyo ya kawaida Mwenyekiti wa
kijiji cha Kilombero 1 Kata ya Rwamgasa Wilayani Geita
amejikuta akisusia kikao cha ndani kilichoitishwa na Mkuu wa wilaya
hiyo ambacho kilikuwa na lengo la kuleta suluhu baada ya
wananchi kudaiwa kufunga ofisi ya kijiji kwa kile kilichoelezwa kuwa kuna
ubadhirifu wa fedha za wananchi ambazo zilitolewa na mwekezaji wa mgodi mdogo
wa Bingwa
Mwenyekiti huyo ambaye anatambulika kwa jina
la Mahano Bwitonde ameshindwa kufika kwenye
kikao hicho kilichokuwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama
ya wilaya sababu ikiwa ni kutokomea na sh. Milioni moja
fedha iliyotolewa na mwekezaji kwa ajili ya kikao cha wajumbe wa serikali ya
kijiji hicho.
Imeelezwa kuwa Mwenyekiti
huyo akiwa na Mtendaji wake wa Kijiji Suzana Chelehani walifika
katika mgodi wa Bingwa unaomilikiwa na Mwekezaji Mwananyanzala Husseni wakiomba
posho kwa ajili ya kikao cha kumjadili na kumkaribisha katika kijiji hicho kama
mwekezaji wa madini ya dhahabu kama ambavyo wamebainisha wajumbe wa serikali ya
Kijiji hicho
No comments:
Post a Comment