Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Huduma za Jamii, imesema mpaka kufikia Februari mwaka huu, Serikali
ilikuwa imetoa Sh bilioni 576.52 pekee kati ya Sh trilioni 1.07 zilizokuwa
zimetengwa kwaajili ya Bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na
Watoto kwa mwaka wa fedha 2017/18, huku bajeti ijayo ikiwa imepungua kwa Sh
bilioni 171.6.
Mwenyekiti wa kamati hiyo,
Peter Serukamba, akisoma maoni ya kamati yake baada ya Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, kusoma makadirio ya
mapato na Matumizi ya Wizara yake, alisema fedha hizo zilizotolewa ni asilimia
53 tu ja bajeti yote iliyopitishwa na Bunge.
Alisema pia kati ya
fedha zilizotolewa, Sh bilioni 190.75 ni za matumizi ya kawaida ya wizara.
“Uchambuzi wa kamti
umebaini fedha zilizotengwa kwaajili ya utekelezaji wa shughuli wizara kwa
mwaka wa fedha 2017/18, ni kiasi kidogo amcho hakiridhishi na kinyume na
matarajio ya Mpango wa Bajeti ambao Bunge na Serikali tulikubaliana,” alisema.
Kwa upande mwingine,
bajeti ijayo ya wizara ya Afya imepungua kw Sh bilioni 171.6 ikilinganishwa na
ile inayoishia Juni 30.
Akisoma hotuba bungeni
jana, Waziri Mwalimu alisema kwa mwaka wa fedha ujao, wizara yake inaomba
kuidhinishiwa na Bunge Sh bilioni 898.374 ikilinganishwa na Sh trilioni 1.07.
No comments:
Post a Comment