Mwenge wa uhuru
umeliza mbio zake Mkoani Geita na kukabidhiwa mkoa wa Kagera huku miradi
mitano ikishindwa kuzinduliwa kutokana na taarifa ya gharama za miradi hiyo
kutofautiana na ya Mkoa.
Akisoma taarifa ya
shughuli za mbio za mwenge wa uhuru zilivyofanyika Mkoani Humo,Mkuu wa Mkoa wa
Geita Mhandisi Robert Gabriel amesema jumla ya miradi sitini na
tatu yenye thamini ya sh ,bilioni 12.7 imepitiwa na mwenge wa uhuru
huku mitano ikishindwa kuzinduliwa serikali ikiendelea na
uchunguzi kubaini tatizo la miradi ambayo haikuzinduliwa na kwamba
tayari TAKUKURU wamekiwisha kuagizwa kufanya uchunguzi wa kina kwenye miradi
hiyo.
Sanjali na hayo
Mhandisi Robert Gabriel ameelezea mmomonyoko wa maadili ambavyo
umeendelea kulikumba Taifa na kwamba kupitia mbio hizo awana budu kuendelea
kukemea na kulaani vitendo hivyo ambavyo vimekuwa vikiwaelemea zaidi
vijana ambao ni nguvu kazi ya Taifa.
Aidha Kiongozi wa mbio
za Mwenge wa uhuru Kitaifa ,Charles Kabeho amempongeza Mkuu wa Mkoa wa
Geita kwa namna ambavyo wameweza kutumia fedha za lipa kutokana na matokeo sasa
kwa kujenga majengo mazuri ya madarasa kwa Bei nafuu Zaidi.
Mkuu wa mkoa wa
Kagera Meja jenerali mstaafu Salum Kijuu amesema miradi ambayo itapitiwa
na mwenge wa uhuru ni 80 na thamani yake ni bilioni 11 na halmashauri
nane ndizo ambazo zitapitiwa.
Mwenge wa uhuru
umeanza mbio zake leo Mkoani Kagera ambapo utakimbizwa kwenye
halmashauri nane huku kauli mbiu ikiwa ni elimu ni ufunguo wa maisha
wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu.
No comments:
Post a Comment