Waziri Wa
Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ''Vyandarua
bure kwa Wajawazito na Watoto,atakaeuza kukiona''.Waziri Ummy akizungumza leo
kwenye ugawaaji wa Vyandarua katika Zahanati ya Mwandiga mapema leo,mkoani
Kigoma.
Waziri Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee
na Watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi chandarua chenye dawa ya muda mrefu Mwantum
Mohammed baada ya kuzindua kuzindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa
ya muda mrefu kwa akinamama wajawazito na watoto wenye umri wa mwaka mmoja,
mpango ambao unaendeshwa na shirika la Johns Hopkins kupitia mradi wa Vectors
Work chini ya ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana
na Malaria. Kulia ni mwakilishi wa USAID Tanzania Andy Karas.
Mwakilishi wa USAID Tanzania Andy Karas
akimkabidhi chandarua chenye dawa ya muda mrefu Asha Juma baada ya uzinduzi wa
ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa akinamama
wajawazito na watoto wenye umri wa mwaka mmoja, mpango ambao unaendeshwa na
shirika la Johns Hopkins kupitia mradi wa Vectors Work chini ya
ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa kupambana na
Malaria.
Waziri Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwasikiliza akinamama wanaudhuria kliniki kwenye Zahanati ya Mwandinga Wilaya ya Kigoma Vijijini baada ya kuzindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa akinamama wajawazito na watoto wenye umri ya mwaka mmoja mpango ambao unaendesha na shirika la Johns Hopkins kupitia mradi wa Vectors Work chini ya ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Raisi wa Marekani wa kupambana na Malaria.
Waziri Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee
na Watoto Ummy Mwalimu akiwasikiliza akinamama wanaudhuria kliniki kwenye
Zahanati ya Mwandinga Wilaya ya Kigoma Vijijini baada ya kuzindua kuzindua
ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa ya muda mrefu kwa akinamama
wajawazito na watoto wenye umri ya mwaka mmoja mpango ambao unaendeshwa na
shirika la Johns Hopkins kupitia mradi wa Vectors Work chini ya
ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Raisi wa Marekani wa kupambana na Malaria.
Waziri Wa Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee
na Watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi chandarua chenye dawa ya muda mrefu Mwantum
Mohammed baada ya kuzindua kuzindua ugawaji endelevu wa vyandarua vyenye dawa
ya muda mrefu kwa akinamama wajawazito na watoto wenye umri ya mwaka mmoja
mpango ambao unaendesha na shirika la Johns Hopkins kupitia mradi wa
Vectors Work chini ya ufadhili wa USAID kupitia mfuko wa Rais wa
Marekani wa kupambana na Malaria.
Waziri Wa
Afya maendeleo ya Jamiii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameagiza Waganga
Wakuu Wa Mikoa,Wa Wilaya na Waganga Wafawidhi kuweka Matangazo katika Vituo vya
Afya, Zahanati na Hospitali kwamba huduma za upimaji na Matibu ya Malaria ni
bure na Wananchi hawatakiwi kulipia kwakuwa kuna wafadhili wanao gharamia
gharama hizo.
Maagizo hayo aliyatoa
jana Mkoani Kigoma katika Zahanati ya Mwandiga Wakati akizindua ugawaji wa
Vyandarua endelevu vyenye dawa ya Muda mrefu ,kwa Wakina Mama wajawazito na
Watoto wenye umri wa Mwaka Moja wa ushirikiano wa Serikili ya Tanzania kupitia
wizara ya afya kitengo cha kudhiti malaria na Shirika la misaada la marekani
(USAID) ambapo alipokea Malalamiko kutoka kwa Wananchi wakidai kutozwa fedha
kwaajili ya Matibabu na Wakati serikali imeagiza Zoezi hilo ni bure.
Waziri Mwalimu alisema
Ugawaji endelevu wa Vyandarua ni mradi unaoendeshwa kwa pamoja na shirika la
JohnsHopkins Center for Communication na Vectorworks kwa ufadhili wa shirika la
misaada la Marekani (USAID) kupitia mfuko wa Rais wa Marekani wa Kudhibiti
malaria Na kuratibiwa na Serikali kupitia Mradi wa Kupambana na Malaria NMCP
kwa hiyo vyandarua hivyo ni bure na Wananchi wanatakaiwa wasilipie.
Aidha alisema ofisi ya
takwimu (NBS) katika kaya mwaka 2017 zilionyesha kupungua kwa kiwango cha
Maambukizi ya Malaria hadi chini ya asilimia 10% kutokana na Mikakati
iliyowekwa na Wizara kuhakikisha wanatokomeza ugonjwa wa Malaria.
Alisema mikakati ya Serikali
ni kuongeza kasi ya upimaji wa Malaria kwa kutumia kipimo cha (mRDT) Hadubini
na Kutumia dawa za mseto pindi wanapothibitika kuwa na Vimelea vya malaria ,
kuwapatia Wajawazito Vyandarua vyenye viuatilifu ili kujikinga kuumwa na Mbu
pia kuwapatia dawa za Sp kwa kipindi maalumu wakati wa ujauzito ilikuwakinga na
madhara yatokanayo na Malaria.
"Niendelee
Kusisitiza dawa za malaria na Matibabu ni bure Wananchi hawatakii kulipia,
wafadhiri wetu wanajitoa sana kuhakikisha Suala la Malaria liishe , Waganga
wafawidhi wanatuangusha sana niombe muweke matangazo na namba za simu kwenye
vituo vya Afya iliwananchi watakao lipishwa watoe Malalamiko yao ilikuweza
kuondokana na changamoto ya Ugonjwa wa Malaria", alisema Mwalimu.
Kwa upande wake Mganga
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Vijijini , Elisha Robarti alisema zahanati hiyo
inakabiliwa na upungufu wa Watumishi wahitaji ni watumishi 15 na waliopo ni
watumishi saba hali inayopelekea Watumishi kulemewa.
Wakitoa Malalamiko yao
Wananchi waliofika kupata huduma Katika Zahanati hiyo mbele ya Mh Waziri, Lydia
Leonard alisema Wamekuwa wakitozwa shilingi 2500/= kwaajili ya Kipimo cha
Malaria na kulipa dawa wanapofika kwaajili ya Matibabu .
Alisema pamoja na kuwa
na Kadi ya bima ya Afya lakini bado wanaendelea kutozwa fedha na kumuomba
Waziri kusimamia suala hilo iliwaweze kupata Matibabu bure kama serikali inavyo
elekeza.
Hata hivyo Wananchi hao
Shukuru Issa aliomba Serikali kuwajengea Kituo cha Afya Kata ya Mwandiga pamoja
na kuboreshewa huduma Za Maji kwani maji wanayo yatumia sio salama na
Wanalazimika kutumia Kilomita 13 kufuata huduma na Waziri alitoa maelekezo kwa
halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Vijijini kuanza ujenzi wa kituo hicho
No comments:
Post a Comment