Naibu Waziri wa Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la
Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Wajumbe wa Kikao cha
Baraza hilo kilichofanyika katika Ukumbi wa Wizara yake, mjini Dodoma leo.
Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa
Baraza hilo, Elius Kwandikwa. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani
nchini ambaye pia ni Katibu wa Baraza hilo, Fortunatus Musilimu
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi
Hamad Masauni (katikati meza kuu) akimsikiliza Mjumbe wa Baraza hilo, ambaye
pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi nchini (TABOA), Enea Mrutu
alipokuwa masuala ya usalama barabarani katika kikao cha Baraza hilo
kilichofanyika katika Ukumbi wa Wizara, mjini Dodoma leo. Kushoto meza kuu ni
Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza
hilo, Elius Kwandikwa. Kulia ni Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini
ambaye pia ni Katibu wa Baraza hilo, Fortunatus Musilimu.
Mkuu wa Kikosi cha
Usalama Barabarani nchini ambaye pia ni Katibu wa Baraza la Taifa la Usalama
Barabarani, Fortunatus Musilimu, akimfafanulia jambo Naibu Waziri wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo, Mhandisi Hamad
Masauni (katikati meza kuu), wakati wa kikao cha Baraza hilo lililokua
linajadili masuala mbalimbali ya usalama barabarani. Kikao hicho kilifanyika
katika Ukumbi wa Wizara yake, mjini Dodoma leo. Kushoto meza kuu ni Naibu
Waziri wa Wizara ya Ujenzi, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza hilo,
Elius Kwandikwa.
(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
No comments:
Post a Comment