Baadhi ya wafanyabiashara wadogo Mkoani Geita
wameiomba mamlaka ya mapato nchini (TRA) kuendelea kutoa elimu ya mlipa kodi
kutokana na wengi wao kutokuwa na elimu hiyo hali ambayo imeendelea
kuwafanya kushindwa kutambua maana harisi ya kulipia kodi.
Wakizungumza na storm
habari wafanyabiashara hao akiwemo Mashaka Maige. na Anastazia
Charles wameiomba mamlaka ya mapato nchini TRA kuwatembelea na kuwapatia
elimu Kwani wengi wao awana mwamko wa kulipia
kodi kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha na kwamba kufanya hivyo
kutawasaidia kutambua umuhimu wa kulipa kodi kwenye mamlaka husika.
Aidha afisa
mwandamizi wa huduma ya elimu kwa Mlipa kodi toka makao makuu ya TRA
nchini Bw,Maternus Mallya amesema kuwa tayari wamekwisha kuanza kutoa elimu kwa
baadhi ya maeneo na kwenye Wilaya zilizomo Mkoani humo,Huku Meneja wa TRA
Mkoani Geita James Jilala akisisitiza zoezi la usajili wa Tin namba kwa
wafanyabishara na kwamba kupitia elimu itawasaidia watu kujua maana
harisi ya ulipiaji wa kodi.
No comments:
Post a Comment