Tuesday, 3 April 2018

PICHA : BUNGE LA RIDHIA AZIMIO LA MAKUBALIANO YA PARIS CHINI YA MKATABA WA UMOJA WA MATAIFA




Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba hii leo amewasilisha Bungeni azimio la kuridhia Makubaliano ya Paris chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, Bunge limeridhia azimio hilo leo tarehe 3/4/2018.






Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mhe. Kangi Lugola akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mhe. Innocent Lugha Bashungwa mara baada ya Bunge kuridhia Makubaliano ya Paris chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi.





Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo (kulia) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mhe. Suleiman Sadiq mara baada ya kuahirishwa kwa shughuli za Bunge hii leo.




Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akisisitiza jambo kwa watendaji wa Ofisi yake. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph Malongo na Bi. Butamo Phillip Naibu Katibu Mkuu.




No comments:

Post a Comment