Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa nchini
Uingereza Mhe. Penny Mordaunt jijini London. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan(kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa
Maendeleo ya Kimataifa nchini Uingereza Mhe. Penny Mordaunt(kushoto) jijini
London.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Maendeleo ya
Kimataifa nchini Uingereza Mhe. Penny Mordaunt na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Agustine Mahige jijini
London.
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(kulia) akipokelewa
na Balozi wa Tanzania Nchi Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro alipowasili
jijini London.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini kitabu cha wageni mbele ya Balozi wa Tanzania Nchi Uingereza Dkt. Asha-Rose Migiro jijini London. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amkutana na
kufanya mazungumzo na Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa nchini Uingereza
Mhe. Penny Mordaunt.
Makamu wa Rais ambaye
amewasili nchini Uingereza leo kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa
Serikali wa Jumuiya ya Madola (CHOGM) akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Katika mkutano wake na
Waziri huyo wa Uingereza Makamu wa Rais alielezea hatua kubwa iliyofikiwa na
Serikali ya Awamu ya Tano katika Elimu mara baada ya kuamua Elimu iwe bure
kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha nne.
Pia Makamu wa Rais
alishukuru mradi wa DFID unatekelezwa mkani Simiyu na kuomba mradi huo
uongezewe maeneo ili uweze kuwanufanisha watoto wengi wa kike.
Makamu wa Rais pia
alizungumzia namna Majukwaa ya Kuwawezesha wanawake kiuchumi yanavyofanya kazi
huku taratibu mbali mbali zinafanyika ili mabenki yaweze toa mikopo kwa riba
nafuu.
Mwisho Makamu wa Rais
alizungumzia jitihada mbali mbali zinazofanywa na Serikali katika kuboresha
Mazingira ya kufanya Biashara nchini.
Naye Waziri wa Maendeleo
ya Kimataifa nchini Uingereza Mhe. Penny Mordaunt ameipongeza Serikali ya Awamu
ya Tano kwa jitihada wanazofanya katika kuboresha huduma za kijamii, alisema
nchi yake ipo tayari kusaidia katika masuala ya makusanyo ya kodi, kuboresha
uwezo wa walimu kwa kuwapatia mafunzo mbalimbali.
No comments:
Post a Comment