Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu
akionyesha rasmi Matokeo ya Utafiti wa Viashiria vya Malaria kwa Mwaka 2017
hapa nchini baada ya kuzindua wakati wa maadhimisho ya siku ya malaria ambayo
yamefanyika Kasulu Mkoani Kigoma. Wengine ni Waziri wa Elimu Joyce Ndalichako –
kwanza kulia, Balozi wa Uswizi ha Tanzania Florence Tinguell na Naibu Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Halima Maulid na Mwakilishi Mkazi wa USAID
Tanzania Andy Karas.
Waziri wa Afya Maendeleo ya jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu
akimkabidhi Waziri wa Elimu Joyce Ndalichako Matokeo ya Utafiti wa Viashiria
vya Malaria kwa Mwaka 2017 hapa nchini baada ya kuzindua wakati wa maadhimisho
ya siku ya malaria ambayo yamefanyika Kasulu Mkoani Kigoma. Wengine ni– kwanza
kushoto Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Halima Maulid na na
Mwakilishi Mkazi wa USAID Tanzania Andy Karas.
Waziri wa
Afya Maendeleo ya jamii Jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu akimkabidhi
Mwakilishi Mkazi wa USAID Tanzania Andy Karas.Matokeo ya Utafiti wa Viashiria
vya Malaria kwa Mwaka 2017 hapa nchini baada ya kuzindua wakati wa maadhimisho
ya siku ya malaria ambayo yamefanyika Kasulu Mkoani Kigoma. Kulia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Ofisi ya Takwimu Tanzania – NBS Albina Chuwa.
Picha ya pamoja ikiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiwa na viongozi wa Serikali na
viongozi wa mashirika mbali mbali ya kimataifa, wakiwa katika viwanja vya Umoja
Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma katika maadhimisho ya siku ya Malaria duniani.
Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy
Mwalimu kushoto akipokea ramani ya Tanzania inayoonyesha maeneo yaliyopungua
kwa malaria kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dkt. Albina Chuwa
wakati wa maadhimisho ya kilele cha Siku ya Malaria Duniani Mkoani
Kigoma,pichani kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa USAID Tanzania Andy Karas.
Afisa Mradi JOHNS HOPKINS VectorWorks Jacqueline Madundo
akitoa maelezo mafupi kuhusu mfumo unaosimia uwajibikaji katika maswala ya
vyandarua nchini kwa Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati wa kilele cha Maadhmisho ya Malaria
yaliyofanyika leo katika wilaya ya Kasulu Mkoani kigoma ikiwa imebeba kauli
mbiu isemayo "NIPO TAYARI KUTOKOMEZA MALARIA WEWE JE?
Kundi la muziki wa Bongo fleva la WEUSI wakiwa jukwaani kutoa Burudani na Elimu juu ya kinga ya ugonjwa wa Malaria ambayo imehadhimishwa katika viwanja vya Umoja Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma katika maadhimisho ya siku ya Malaria duniani.
Kundi la wananchi lililojitokeza katika viwanja vya Umoja Wilaya ya
Kasulu mkoani Kigoma katika maadhimisho ya siku ya Malaria duniani ili
kusikiliza ujumbe kuhusu Malaria, mgeni rasmi wa tukio hilo ni Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu (MB).
Kikundi
cha ngoma kutoka Umoja Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma kikiburudisha Viongozi na
wananchi waliofika katika viwanja vya Umoja ikiwa ni maadhimisho ya siku ya
Malaria Duniani ambayo kwa mwaka huu yanahadhimishwa leo Aprili 25 katika
Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma
Maambukizi ya viashiria
vya ugonjwa wa Malaria Nchini Tanzania yamepungua kwa Watoto chini ya miaka
mitano kutoka Asilimia 14.4 mwaka 2015 na kufikia asilimia 7.3 kwa Mwaka 2017
hii ni kuzigatia harakati zinazofanywa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na
Mashirika ya Marekani (USAID) pamoja na shirika la WHO kuhakikisha
wanautokomeza ugonjwa huo.
Akizindua takwimu zilizo
tolewa na Ofisi ya Takwimu ya Tanzania leo Wilayani Kasulu Mkoani Kigoma Waziri
wa Afya Maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu , alisema Siku
ya leo kupitia maadhimisho hayo yaliyofanyika kitaifa Kigoma, atazindua rasmi
Matokeo ya Utafiti wa Viashiria vya Malaria kwa Mwaka 2017.
Kwa Mujibu wa Mkurugenzi
mkuu ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Albina Chuwa alithibitisha Matokeo ya sasa ya
utafiti huu, yanaonesha kuwa kiwango cha malaria kwa watoto wenye umri wa chini
ya miaka mitano nchini Tanzania kimeshuka kwa Zaidi ya nusu kutoka asilimia
14.4 mwaka 2015 hadi asilimia 7.3. Hii ni kwa kutumia kipimo cha haraka cha
utambuzi wa vimelea (mRDT).
Waziri Ummy alisema
utafiti huo unaonesha Mikoa yenye kiwango kikubwa cha watoto wenye malaria ni,
Kigoma (asilimia 24.4), Geita (asilimia 17.3), Kagera (asilimia 15.4) na Tabora
(asilimia 14.8) ambapo Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Njombe, Songwe na
Dodoma ina kiwango kidogo cha maambukizi chini ya asilimia moja.
"Takwimu hizi,
zinaonesha kupungua kwa kiwango cha malaria kwa kiasi kikubwa, na hii ni habari
njema kwetu sote na inaonesha ni jinsi gani Serikali yenu ipo tayari kutoa
kipaumbele katika kuhakikisha kuwa malaria inadhibitiwa na hatimae tuweze
kuitokomezwa kabisa Ili kuhakikisha lengo hilo linafanikiwa, tunapaswa kufanya
kazi kwa pamoja katika kufikia malengo tuliyojiwekea ili jamii, hasa watoto
chini ya umri wa miaka mitano na wanawake wajawazito ambao ndio waathirika
wakubwa wa ugonjwa wa malaria waweze kuepukana na ugonjwa huu", alisema
Waziri Mwalimu. Alisema Pamoja na mafanikio makubwa yaliyopatikana, lakini bado
kuna changamoto, ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi ili kwa pamoja tuweze kufikia
malengo ya kutokomeza malaria nchini.
Changamoto hizo ni
pamoja na Wanajamii kutotumia vyandarua ipasavyo katika kujikinga na ugonjwa wa
malaria, kuwepo kwa mitazamo potofu juu afua za kupambana na malaria; mfano
dhana ya kuwa viuatilifu-ukoko za kunyunyizia ukutani zinaleta kunguni na
viroboto na kuwa vyandarua vinapunguza nguvu za kiume ni dhana potofu ambazo
hazina ukweli wowote. Vilevile, Jamii kutoshiriki kikamilifu katika kutunza
mazingira na kuharibu mazaliaya Mbu.
Kwa upande wake
Mkurugenzi mwakilishi wa shirika la misaada na Maendeleo la Marekani USAID Andy
Karas alisema kwa zaidi ya miaka 12 USAID imekuwa ikifanya kazi pamoja na
serikali kupitia Wizara ya Afya kwaajili ya Kupambana na Malaria.
Alisema watoto wengi
walio hai leo ni kwa juhudi za serikali, kwa kushirikiana na Mfuko wa Rais wa
Marekani wa kupambana na Malaria kwa Muda wote wameweza kusambaza vyandarua
zaidi ya milioni 10 na kununua viuwadudu zaidi ya milioni 20 na kupuliza dawa
ya Mbu kwenye maeneo hatarishi vile vile wameweza kushirikiana na ofisi ya
Taifa ya Takwimu kwa kufanya takwimu mbalimbali juu ya kupungua kwa ugonjwa wa
Malaria.
Nae Balozi wa Usizwi
Florence Tinguell aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Wizara
ya Afya kwa juhudi kubwa walizo zifanya katika kuhakikisha wanatokomeza Malaria
,imeweza kubuni mbinu. Kwa zaidi ya miaka 50 Ubalozi wa Uswizi umekuwa
ukifadhili tafiti za malaria ambazo zimekuwa zikifanywa na taasisi ya Ifakara
Health Institute.
Hata hivyo mjumbe wa
kamati ya bunge ya kupambana na Malaria ( TAPAMA) na Mbunge wa Viti maalumu
Mkoa wa Iringa Rose Tweve alisema wao kama wabunge wanatoa wito kwa Wananchi
wote kuwa jukumu la kupambana na Malaria na mapambano dhidi ya Malaria ni la
Wananchi na wasiiachie serikali peke yake na kuomba nguvu kubwa ielekezwe
kwenye kinga na wahudumu wa Afya na wakina mama kufika hospitali kwa wakati
ilikuweza kupatiwa kinga ya Malaria.
Kilele cha Maadhmisho ya
Malaria kimefikia tamati leo kwa kufanyika katika wilaya ya Kasulu Mkoani
kigoma ikiwa imebeba kauli mbiu isemayo "NIPO TAYARI KUTOKOMEZA MALARIA
WEWE JE?
No comments:
Post a Comment