Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na
Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Andrea Barnabas Pembe akizindua kitabu
kwa ajili ya kuwafundishia wanafunzi wanaosoma mwaka wa nne katika fani ya
udaktari hasa wale wa Magonjwa ya Dharura hafra iliyofanyika ukumbi wa ukumbi
wa Kitengo cha Magonjwa ya Dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
jijini Dar es Salaam.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Andrea Barnabas Pembe akizindua kitabu kwa ajili ya kuwafundishia wanafunzi wanaosoma mwaka wa nne katika fani ya udaktari hasa wale wa Magonjwa ya Dharura hafra iliyofanyika ukumbi wa ukumbi wa Kitengo cha Magonjwa ya Dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Tiba ya Dharura na Ajali wa Chuo
Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Dk. Hendry Sawe ambaye
ni mtunzi wa kitabu hicho na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Dharura akipongezwa
na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili
(MUHAS), Andrea Barnabas Pembe mara baada ya kumaliza uzinduzi.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na
Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Andrea Barnabas Pembe na Mkuu wa Idara ya
Tiba ya Dharura na Ajali wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili
(MUHAS) Dk. Hendry Sawe ambaye ni mtunzi wa kitabu hicho na Daktari Bingwa wa
Magonjwa ya Dharura wakimpatia zawadi ya kitabu mmoja ya kiongozi wa wanafunzi
hao.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na
Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Andrea Barnabas Pembe akizindua kitabu
kwa ajili ya kuwafundishia wanafunzi wanaosoma mwaka wa nne katika fani ya
udaktari hasa wale wa Magonjwa ya Dharura hafra iliyofanyika ukumbi wa ukumbi
wa Kitengo cha Magonjwa ya Dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)
jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Tiba ya
Dharura na Ajali wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS)
Dk. Hendry Sawe ambaye ni mtunzi wa kitabu hicho na Daktari Bingwa wa Magonjwa
ya dharura akitoa shukrani zake wa wanafunzi wake ambao wamekuwa msitari wa mbele
kumtia moyo wakati akiandika kitabu chake. Kitabu hicho ni mahususi kwa
wanafunzi wanaosoma mwaka wa nne fani ya udaktari hasa wale wa Magonjwa ya
Dharura.
Wanafunzi waliohudhuria hafla hiyo.
Mshehereshaji wa shughuli akitoa machache.
Picha ya pamoja.
Jamii imetakiwa
kushirikiana vyema na kitengo cha magonjwa ya dharura ya hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH) ili waweze kupatiwa huduma iliyo bora.
Kauli hiyo ameitoa Kaimu
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS),
Andrea Barnabas Pembe wakati akizindua kitabu kwa ajili ya kuwafundishia wanafunzi
wanaosoma mwaka wa nne katika fani ya udaktari hasa wale wa kitengo cha Dharula
hafla iliyofanyika ukumbi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Kitengo cha
Dharula jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa kitengo cha
dharula kwa nchini Tanzania ni kipya sana na kilianza 2010 hivyo kinahitaji
maboresho ya mara kwa mara ili kiwahudumie wananchi vyema.
"Tunaomba wananchi
wawe bega kwa bega na kitengo cha dharula ili kuweza kutoa maoni yao pale
wanapoona hawapewi huduma bora, tunahitaji kila mtu awajibike kwa upande wake
tusikae kimya kuongelea uchochoroni," alisema Pembe.
Aliongeza kuwa kitabu
kilichozinduliwa kitaweza kumjenga mwanafunzi awe imara kwa kujua mengi katika
utoaji wake wa huduma.
"Kitabu hiki
kimeandikwa na Mtanzania ambaye ni Mkuu wa Idara ya Tiba ya Dharura na Ajali wa
Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Dk. Hendry Sawe na
pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya dharura hivyo aliyoyaandika yote ni yale
ambayo amekuwa akiyafanya mpaka yakampa cheo hicho kikubwa, naamini hata
wanafunzi watakao kisoma vile vile watafuata nyayo zake," alisema.
Nae mtunzi mkuu wa
kitabu hicho, Mkuu wa Idara ya Tiba ya Dharura na Ajali wa Chuo Kikuu cha Afya
na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Dk. Hendry Sawe ambaye pia ni Daktari
Bingwa wa Magonjwa ya dharura alisema kuwa wameamua kuandika kitabu hicho ili
kuweza kuwasaidia wanafunzi waweze kupata elimu halisi inayoendana na mazingira
yetu ya kiafrika.
"Katika masomo ya
udaktari kuna vitabu vingi kutoka nje ya nchi ambavyo havimsaidii mwanafunzi
kwa vile vimeandikwa ili vitumike kwa nchi zilizoendela hivyo vinapofika nchini
Tanzania havikidhi kiu ya wanafunzi maana mambo anayokuwa anasoma kama hadithi
za kufikirika," alisema.
Alisema kuwa iko haja ya
watunzi wa vitabu wakajikita kuangalia uandishi bora utakaoweza kumsaidia
mwanafunzi aweze kujikwamua na si kusoma mambo yakufikirika tu.
Kwa upande wake Bingwa
wa Magonjwa ya Dharura, Prof. Victor Mwafongo ambaye ni mwalimu wa Dk. Hendry
alitoa pongezi kwa kijana wake ambaye anasema nyota yake ameendelea kuwaka kila
kukicha kwa kubuni njia mbali mbali za kuwasaidia wanafunzi.
"Dk. Hendry ni
kijana ambaye walikuwa wanafunzi wangu wa kwanza na leo naona matunda yake kwa
kuendelea kung'aa, na kitabu alichokiandika kitawasaidia sana wanafunzi
wanaosoma masomo ya dharura," alisema.
No comments:
Post a Comment