Kaimu Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao cha kazi na wakuu wa idara, vitengo na wafanyakazi wote wa NFRA Mkao makuu Mjini Dodoma
Wakuu wa idara, vitengo na wafanyakazi wote wa NFRA Mkao makuu Mjini Dodoma wakifatilia kwa umakini kikao cha kazi kilichoongozwa na Kaimu Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba
Kutoka kushoto ni Meneja Rasilimali watu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Fredy Mbonde, Afisa Ugavi NFRA Magreth Salia Kavishe, na Mhandisi Imani Nzobonaliba ambaye ni Mhadisi Mwandamizi NFRA wakifatilia kwa umakini kikao cha kazi kilichofanyika katika Ofisi za NFRA Mtaa wa Kizota Mjini Dodoma
Mhandisi Imani Nzobonaliba ambaye ni Mhadisi Mwandamizi NFRA na Mratibu wa Mradi wa kuongeza uwezo wa uhifadhi wa wakala wa Taifa wa hifadhi ya chakula, akiwasilisha maelezo mafupi ya namna mradi utakavyotekelezwa wakati wa kikao kazi cha wakuu wa idara, vitengo na wafanyakazi wote wa NFRA
Kaimu Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba (Kulia) akisisitiza jambo wakati akizungumza kwenye kikao cha kazi na wakuu wa idara, vitengo na wafanyakazi wote wa NFRA Mkao makuu Mjini Dodoma, Mwingine pichani ni Mkurugenzi wa maendeleo na Bishara wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Ndg Mikalu Mapunda
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe
Kasim Majaliwa (Mb) anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za uwekaji wa
jiwe la msingi kwa mradi wa kuongeza uwezo wa uhifadhi wa wakala wa Taifa wa
hifadhi ya chakula katika dhifa itakayofanyika kwenye viwanja vya Ofisi za
Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula zilizopo Mtaa wa Kizota Mjini Dodoma.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Afisa Mtendaji mkuu
wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba wakati
akizungumza kwenye kikao cha kazi na wakuu wa idara, vitengo na wafanyakazi
wote wa NFRA Mkao makuu Mjini Dodoma.
Bi. Zikankuba ameeleza kuwa Mradi huo utagharimu Dola za
Kimarekani Milioni 55, ikiwa ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali ya
Poland ikiwa ni sehemu ya kiasi cha milioni 110 kilichotolewa kwa serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha, amesisitiza kuwa mikataba ya ujenzi ilianza kufanya kazi
tarehe 9 Disemba 2017 huku akisema Mradi huo utatekelezwa na kampuni mbili za
Kandarasi kutoka Poland ambazo ni (Feerum S.A na Unia Araj Realizacje Sp.o.o)
ambapo msimamizi wa utekelezaji wa mradi ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).
Alisema Mradi utahusisha ujenzi wa vihenge vya kisasa, maghala
ya kisasa pamoja na ukarabati wa ofisi na kutekelezwa katika maeneo nane ambayo
ni Arusha (Babati), Dodoma, Makambako, Mbozi, Shinyanga, Songea, Sumbawanga na
Mpanda.
Baada ya mradi kukamilika Wakala utakuwa umeongeza uwezo wa
kuhifahi kwa 250,000 MT zaidi (vihenge vya kisasa 190,000MT na maghala 60,000
MT) jambo ambalo litakuwa chachu na mafanikio yenye tija katika kuunga mkono
Juhudi za utendaji wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli.
Alisema kupatikana kwa Mradi huo nchini ni
jitihada za Serikali ambazo zitapelekea ukuaji wa uchumi nchini na kuchangia
kuwezesha Tanzania ya viwanda ambapo kutawezesha maghala ya Wakala kuweza
kuhifadhi akiba ya Chakula ambayo itaendana na mahitaji halisi ya dharura
kulinganisha na ongezeko la watu nchini.
Hifadhi ya Chakula
inayohitajika kukidhi mahitaji ya dharula kwa miezi mitatu ni zaidi ya tani
500,000 ukilinganisha na tani 150,000 iliyokuwa inahitajika miaka ya 1992
Wakala ulipoanzishwa.
Pia, technologia ya
vihenge itawezesha Wakala kutumia teknolojia ya kisasa na hivyo kupunguza
gharama za uendeshaji, Itawezesha Wakala kuhifadhi chakula kwa muda mrefu Zaidi,
itasaidia kupunguza upotevu wa zao la mahindi baada ya kuvuna (posthaverst
loss) na kuongeza soko la mahindi nchini na kuimarisha usalama wa nafaka
inayohifadhiwa kwa kudhibiti sumukuvu (Aflatoxin) kwa mahindi yaliyohifadhiwa.
Katika kikao kazi
hicho Kaimu Afisa Mtendaji mkuu wa Wakala wa
Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Bi Vumilia L. Zikankuba amewasihi
wafanyakazi wote wa NFRA kufanya kazi kwa ushirikiano na kutambua kuwa nidhamu
na bidii yao itakuwa chachu ya mafanikio zaidi katika kuimarisha utendaji wa
NFRA.
No comments:
Post a Comment