Thursday, 5 April 2018

WAKULIMA KUNUFAIKA NA KILIMO CHA PAMBA MKOANI GEITA

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa  uhuru Kitaifa Charles Kabeho akizungumza na kuwasisitiza wakulima wa zao la Pamba kuwekaza nguvu zaidi kulima zao hilo wakati alipoweka Jiwe la Msingi kwenye mradi wa shamba la pamba kijiji cha Nyamalimbe Wilayani Geita.

Baadhi ya pamba zikiwa shambani kabla ya kuvunwa.







Kiongozi wa mbio za Mwenge wa  uhuru Kitaifa Charles Kabeho,akiweka jiwe la msingi kwenye shamba la pamba kwenye kijiji cha Nyamalimbe.

Watoto ambao ni yatima wakipewa zawadi na Kiongozi wa mbio za mwenge Charles Kabeho  kwenye Kijiji cha Bujura wilayani Geita.






Serikali imewahakikishia mazingira yaliyo salama wakulima wa zao la pamba ikiwa ni pamoja na kununuliwa kwa zao hilo bila ya kukopwa kwa  msimu wa pamba ambao unatarajia kuanza tarehe 1 Mei mwaka huu .


Hayo yameelezwa  na kiongozi wa mbio za mwenge wa  uhuru , Charles Kabeho wakati akifungua mradi wa zao la pamba katika kijiji cha  Nyamalimbe Halmashauri ya Wilaya ya  Geita ambapo alisema  serikali imejipanga kuhakikisha mkulima wa pamba mwaka huu ananufaika na zao hilo.

“ Zao la Pamba linamanufaa kwa mkulima na serikali kwani zao ambalo  linatengeneza nguo kuliko kusubili kuletewa mitumba kutoka nje hivyo tulithamini zao hili kwani linasaidia pia kuondoa umaskini katika familia”Alisisitiza Kabeho.

Mussa Kabehe ambaye ni Mkulima wa zao hilo alisema kwa sasa kutokana na hali ya hewa na mvua kunyesha kwa wingi wamekuwa na matumaini machache ya kupata pamba Nyingi kwani asilimia kuwa zimeharibikia shambani na kwamba awana matarajio ya kuzalisha pamba Nyingi zaidi ingawa kwa mwaka huu wengi walijitokeza kulima pamba.

Kiongozi huyo wa mwenge pia amefungua miradi  12 katika Halmashauli ya Wilaya ya Geita  iliyo gharimu  kiasi cha shilingi bilioni tano na milioni miatatu ambapo pia kiongozi huyo  aliwakumbusha wananchi wa kijiji hicho kutojihusisha na  suara la rushwa kwa ni adui wa haki.








No comments:

Post a Comment