Baadhi ya wachimbaji wadogo wakifuatilia mafunzo ambayo yalikuwa yanatolewa na wakala wa afya na usalama mahari pa kazi na ofisi za Afisa madini Mkoa wa Geita. |
Kaimu meneja wa wakala wa afya na usalama mahari pa kazi Bw,Mjamo Mohamed akisoma taarifa ya semina hiyo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Geita. |
Kamishina msaidizi wa madini kanda ya ziwa Viktoria Yahaya Samamba akizungumzia juu ya semina hiyo na faida ambazo watazipata wachimbaji kutokana na mafunzo ambayo watapatiwa. |
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akimkaribisha Mkuu wa Mkoa kwaajili ya kuzungumza na wachimbaji wadogo Mkoani Humo wakati wa semina iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Moyo wa Huruma. |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Geita ,Leornad Bugomola akielezea tatizo la Kabon kuendelea kusafirishwa kwenda Jijini Mwanza. |
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Gabriel akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini Mkoani hapa |
Kipindi cha kuanzia
Julai 2017 hadi Machi 2018 wachimbaji wadogo Mkoani Geita wameripotiwa
kuzalisha kiasi cha Kg. 68.55 zenye Thamani ya TSh. Bilioni 6.5 ongezeko hilo
la uzalishaji linatokana na marekebisho ya Sheria ya Madini ya mwaka 2017
pamoja na kanuni zake za mwaka 2018.
Hayo yamebainishwa na
mkuu wa mkoa wa Geita mhandisi Robert Gabriel wakati alipokuwa akifungua
mafunzo ya siku moja yaliyokuwa yamelenga kuwawezesha wachimbani wadogo
kutambua mbinu za kujikinga na ajali zinazotokana na mvua ambazo zinaendelea
Kunyesha.
Mheshiwa Gabriel
amesema serikali itaendelea kusimamia na kukusanya mrabaha na tozo kwa kufuata
utaratibu wa sheria ambazo zinawataka wachimbaji wadogo kulipa tozo kutokana na
shughuli ambazo wanazifanya kwenye maeneo hayo.
Miongoni kati ya mambo
ambayo yameonekana ni changamoto ni usafirishaji wa kaboni ya kuchenjuliana
madini ya dhahabu kwenda mwanza ambapo Mkuu huyo amesema wanatarajia
kutoa matangazo ya kuzuhia shughuli hiyo ya kusafirisha kaboni na kwamba
itatumika ndani ya mkoa huo kutokana na mapato ambayo yameendelea kupotea.
Kamishina msaidizi wa
madini kanda ya ziwa Viktoria Yahaya Samamba amesema mapendekezo hayo ni mazuri
na kwamba watakaa na wamiliki wa makarasha ili waweze kuwashauri kuwa na
mashine ambazo zitasaidia wachimbaji wadogo kutokupeleka kaboni mwanza na
shughuli hizo zitakuwa zikifanyika Mkoani humo.
Aidha kwa upande wake kaimu
meneja wa wakala wa afya na usalama mahari pa kazi Bw. Mjamo
Mohamed alisema kuwa wameamua kukaa na wachimbaji kutoa semina ya
kujikinga na majanga kwenye maeneo yao ya kazi kutokana na mvua ambazo
zimeendelea kunyesha hivyo kufanya hivyo kutawasaidia kuepukana na majanga
ambayo yanaweza kusababisha watu kupoteza Maisha.
Hata kwa kwa upande wa
mmoja kati ya wachimbaji wadogo ambaye amezungumza na mtandao huu, ameishukuru
ofisi ya madini mkoani humo pamoja na wakala wa afya na usalama mahari pa kazi
kuendesha semina hiyo na kwamba imewajenga na pia imewapa mwangaza kwani
wametambua namna ambavyo wanaweza kujikinga na majanga kwenye maeneo yao ya
kazi ikiwa ni pamoja na kuwapima afya watu ambao wanawaajili kwenye shughuli
zao.
No comments:
Post a Comment