Serikali imesema
itaendelea kuvifuatilia na kuvifungia vyuo vikuu vinavyotoa elimu bila
kuzingatia miongozo, kanuni na sheria zilizowekwa.
Kauli hiyo imetolewa leo
Aprili 27, 2018 na Naibu Waziri wa Elimu, William Ole Nasha wakati akijibu
swali la nyongeza Mbunge wa Viti Maalumu, Ester Mmasi lililoulizwa kwa niaba
yake na mbunge wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi.
Katika swali hilo la
nyongeza, Shangazi aliuliza udhibiti wa Serikali katika vyuo vinavyotoa elimu
bila kufuata miongozo.
Akijibu swali hilo Ole
Nasha amesema mwaka huu Serikali imevifungia vyuo 19, kusitisha programu 75 za
vyuo 19.
“
Tumekuwa tukiielekeza tume ya vyuo vikuu kudhibiti ubora wa elimu ili
kuhakikisha taratibu zote zinafuatwa. Pia Serikali tumekuwa tukizingatia uhuru
wa vyuo hivi lakini tumekuwa tukivifuatilia kuhakikisha kuwa utendaji wake
unazingatia taratibu tulizoziweka,” amesema.
No comments:
Post a Comment