Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith
Shayo akizungumza kuhusu UNESCO inavyoshiriki moja kwa moja kwenye jamii hasa
kuzisadia Radio za kijamii ili kufanya kazi zake kifanisi wakati wa kufunga
mafuzo ya mafundi mitambo kutoka redio jamii 25 zilizopo Tanzania Bara na
Zanzibar yaliyofanyika kwa siku saba katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam. Mafunzo haya ya siku saba yameratibiwa na Shirika la Umoja
wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ufundi kutoka TBC,
Joseph Kambanga akizungumza namna TBC ilivyojitolea kuzisaidia Radio za kijamii
ili kuimarisha upatikanaji wa habari na hata kuimarisha mitambo ya urushwaji wa
matangazo kwenye jamii haraka wakati kufunga mafuzo ya mafundi mitambo
kutoka redio jamii 25 zilizopo Tanzania Bara na Zanzibar yaliyofanyika kwa siku
saba katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Mafunzo kutoka Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Rose Mwalongo
akisisitiza umoja wa mafundi mitambo waliopata mafunzo ili kuweza kufikia
malengo waliyojiwekea wakati wa kufunga mafunzo hayo.
Fundi Mitambo wa Redio Jamii Orkonerei FM,
Baraka David Ole Maika akitoa shukrani kwa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) pamoja na Shirika la
utangazaji la Tanzania(TBC) kwa kuweza kutoa mafunzo kwa mafundi mitambo kutoka
redio jamii 25 yalifanyika kwa Siku saba katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa Mafunzo kutoka Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Rose
Mwalongo(wa kwanza kushoto) pamoja na walimu waliotoa mada mbalimbali katika
mafunzo kwa mafundi mitambo wakiwa kwenye mkutano wa kufunga mafunzo hayo.
Baadhi ya mafundi mitambo wa radio za kijamii 25
wakifuatilia mada wakati wa kufunga mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyofanyika
kwa siku saba katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa na kuratibiwa na Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).
Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo
(kushoto) akiwakabidhi vyeti baadhi ya mafundi mitambo kutoka radio za kijamii
25 za hapa nchini. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ufundi kutoka TBC,
Joseph Kambanga.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ufundi kutoka TBC,
Joseph Kambanga (kushoto) akiwakabidhi vyeti vya kuhitimu kwa baadhi ya mafundi
mitambo kutoka radio za kijamii 25 kutoka Tanzania Bara na visiwani.
Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith
Shayo akiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu ambao ni mafundi mitambo kutoka
radio za kijamii 25 mara baada ya kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku
saba.
No comments:
Post a Comment