Wakazi wa kata ya Mganza
wilayani Chato mkoani Geita wameipongeza Serikali kwa kujenga soko la kimataifa
la uzaji wa samaki na dagaa la kasenda kwani limesaidia kuzalisha Ajira mpya
kwa baadhi ya wanawake na vijana wilayani humo.
Wakizungumza na mwandishi
wetu kwa nyakati tofauti baadhi ya wananchi wa kata hiyo wamesema kuwa kabla ya
kujengwa kwa soko hilo hawakuwa na uhakika wakuingiza kipato kwa siku tofauti
na sasa ambapo wameanza kunufaika.kupitia ajira za kupakia na kuchambua dagaa.
Diwani wa kata ya mganza
Bw.Emanuel Mwita amesema kupitia soko hilo wananchi wake ambao hawakuwa na kazi
maalum sasa wamepata kazi sokoni hapo ambazo zinawaingizia
kipato cha kuendesha maisha ya familia zao.
Katika hatua nyingine Bw
Mwita ameahidi kuishawishi serikali kuweza kuongeza majengo katika soko hilo
yatakayosaidia kuzarisha ajira kwa watu ambao hawajabahatika kupata kazi ya
kufanya katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment