Mwenyekiti wa Kijiji cha Mapinduzi Wilayani
Chato mkoani Geita Bw. Kitute Kalegea amesema hata mvumilia mtu atakaye shindwa
kusafisha Mazingira kwa kufyeka nyasi na kufukia madimbwi ya maji kwa lengo la
kuendelea kutokomeza mazalia ya mbu waenezao ugonjwa wa malaria.
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na Storm
Habari kijijini humo ambapo amesema kuwa ugonjwa wa Malaria katika
kijiji hicho umeendelea kuwa tishio kutokana na baadhi ya wananchi kushindwa
kuzingatia suala la usafi wa mazingira ikiwemo kuharibu mazalia ya mbu waenezao
Ugonjwa huo.
Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo ameahidi
kuwachukulia hatua za kisheria baadhi ya watu wanaotumia vyandarua vya
kujikinga na mbu kwa matumizi yasiyo sahihi ikiwemo kufugia kuku.
Aidha baadhi ya Wananchi katika Kijiji hicho
wameiomba Serikali kuendelea kutoa Elimu ya matumizi sahihi ya Vyandarua
hususani Vijijini ili kuendelea kupambana na kutokomeza maambukizi ya Ugonjwa
huo.
No comments:
Post a Comment