Waziri wa Nchi OR TAMISEMI Mhe. Seleman Jafo
(Mb), akizungumza wakati wa uzunduzi wa mnara wa kuenzi uzalendo wa Mhe.
Rais wa awamu ya tano wa Tanzania katika chuo cha Hombolo.
Baadhi ya watendaji wa Chuo cha Serikali za Mitaa cha Hombolo wakati wa zoezi la uzinduzi wa mnara wa fikra za kizalendo za Mhe. Rais Magufuli
Kikundi cha Ngoma za asili cha Swala kitoa
borudani wakati wa wa uzunduzi wa mnara wa kuenzi uzalendo wa Mhe. Rais
wa awamu ya tano wa Tanzania, kikundi hicho kinachopatikana katika Kijiji cha
Nkoyo, Hombolo ambacho ni maarufu katika mkoa wa Dodoma hususani kudumisha
utamaduni wa mtanzania.
Mwonekano
wa Mnara wa Magufuli Square, Sehemu iliyojengwa mahususi kwa ajili ya kuenzi
uzalendo wa Mhe. Rais John Pombe Magufuli kwa vitendo
Bodi ya Chuo cha Hombolo iliyo maliza muda wake wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa mnara wa fikra za kizalendo za Mhe. Rais Magufuli.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
Selemani Jafo amesema kuanza kwa kozi za ngazi ya Shahada katika Chuo cha
Serikali za Mitaa Hombolo kisiwe kigezo cha kuondosha kozi za Astashahada na
Stashahada katika chuo hicho.
Waziri Jafo alikuwa
akizundua rasmi Bustani ya Magufuli katika chuo hicho ambapo Bustani hiyo
itatumika kuishi na kuenzi mchango wa kiongozi huyo wa Nchi kwasasa ambao ni
uzalendo, kujituma pamoja na uadilifu katika kuwatumikia wananchi.
“Nimesikia maombi yenu
yakutaka Kuanzishwa kwa kozi za Ngazi ya Shahada kusudi mtu anapo hitimu masomo
yake ya ngazi za awali aweze kuendelea, naomba niwambie, tutajitahidi
lifanikiwe, lakini angalizo langu kwenu, tutakapo anzisha Degree isiwe sababu
yakusitisha kozi zinazoendelea kwa sasa, ikiwepo Astashahada (Certificate) na
Stashahada (Diploma) ya kozi mnazo endelea nazo” amesema Jafo.
Waziri Jafo amesema,
vyuo vingi vilipo anzisha ngazi ya Shahada na kusahau wataalam wa kada za kati
vilichochea kukosekana kwa wataalam wakutosha katika ngazi ya kati hususan
mafundi mchundo ambao walikuwa wakizalishwa katika vyuo hivyo.
Katika hatua nyingine
Waziri Jafo amewahakikishia Wakurufunzi hao wa chuo cha Hombolo uhakika wa
kuajiriwa na Serikali kwa wale watakao fikia vigezo vinavyo hitajika katika
nafasi mbali mbali ambazo serikali itatangaza.
“Tumebaini Wataalam wa
chuo cha Hombolo tunaowaajiri katika kada za Maafisa Watendaji wa Vijiji,
Kata na hata Tarafa wanauelewa mpana wa Masuala ya jamii za watanzania hususan
ni wale waishio vijijini, hivyo basi tunapotangaza ajira kipaumbele tutakitoa
kwa wanafunzi wa chuo hiki” amesema Waziri Jafo.
Mhe. Jafo hakusita
kuonesha furaha yake kwa jinsi chuo hicho kilivyo jizatiti katika suala la
utunzaji wa mazingira, hatua ambayo ameitaja ni kumuunga mkono Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye kupitia
Wizara ya Mazingira na Muungano amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha watanzania
wanantunza mazingira.
Mbali ya pongezi hizo
Waziri ametoa maelekezo kwa uongozi wa Manispaa ya Dodoma kuanza kampeni
ya upandaji wa miti ya Matunda. “Tunataka Dodoma iwe Fruit City” amenukuliwa
Waziri
Kwa Upande wake
Mwenyekiti wa Bodi inayomaliza Muda wake Prof. Suleiman Ngware, yeye alisema
lengo la kujenga Bustani ya Magufuli nikuunga mkono juhudi za Mhe. Rais
katika kusimamia rasilimali za nchi kwa moyo uzalendo na uadilifu wa dhati.
“Mhe. Waziri Shabaha
yakuwa na Bustani ya aina hii yenye Mnara wa Magufuli nikutambua mchango mkubwa
na moyo wa kizalendo alionao Rais wetu, sasa tunachotaka nini hapa, kila mtu
atakaye uangalia mnara huu aweze kujitathmini mwenyewe bila yakusukumwa na mtu,
Je! Mimi kama Mkufunzi ninatimiza wajibu wangu? Mimi kama Mwanafunzi nafanya
matendo sawa na Rais wangu? Mimi kama Mwenyekiti wa Bodi au Mkuu wa Shule
sifanyi manyanyaso kwa watu sibagui watu nk, nk" Amesema Mwenyekiti
huyo.
Kila Mwaka ifikapo
Aprili 18, Bodi, Uongozi, Wanafunzi na Wananchi wanaozunguka eneo la chuo
watakuwa wakikutana kwa pamoja na kujitathmini kwa mienendo na matendo yao ya
utendaji wa mwaka mzima, Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo kwa sasa
kinawanafunzi zaidi ya 3000.
No comments:
Post a Comment