|
Baadhi ya makazi ya watu yakiwa yamejaa maji kwenye mitaa ya Mwatulelo Kata ya Buhalahala Mjini Geita kutokana na mvua ambazo zinaendelea Kunyesha. |
Wananchi
wakipita kwa shida kwenye barabara za mitaa ya Mwatulelo kutokana na mvua
ambazo zinaendelea Kunyesha Mkoani Geita.
|
Nyumba ikiwa imeezuliwa paa na kuanguka kutokana na mvua ambazo zinaendelea kunyesha Mkoani Geita.
Mvua
zinazoendelea Kunyesha Mkoani Geita zimesababisha maafa ya vifo vya
watu saba (7) watano wakitokea kwenye halmashauri ya wilaya ya
Nyang’wale na wawili kwenye halmashauri ya Mji wa Geita.
Watu hao wamefariki
kutokana kujaa maji mto ambao upo kwenye mpaka wa Wilaya ya
Nyang’whale na Sengerema huku mtu mmoja akiagukiwa na ukuta wa
Nyumba na mwingine akifariki kutokana na kusombwa na maji .
Akizungumza kwa njia
ya Simu na mtandao huu Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Hamim Gweyama
amesema hadi sasa mwili ambao umetambuliwa na ndugu ni mmoja na
kwamba wanaendelea na jitihada za kutafuta miili mingine kwenye Mto huo.
Aidha kwa upande wake
Mkaguzi msaidizi wa Jeshi la zima Moto na uwokoaji Mkoani Humo Stanley
Paschal akizungumza na waandishi wa habari amesema watu hao wawili
miongoni mwao ni mtoto mwenye umri wa miaka minne ambaye anajulikana kwa jina
la Aneth Juma na Mzee Vicent Kipili ambaye aliangukiwa na ukuta ,huku akiwataka
wananchi kuwa waangalizi wa watoto wao kwenye kipindi hiki cha msimu wa mvua.
Kwa upande wa Mashuhuda
wa ajali ya Mtoto huyo Bi. SCOLA SANGA NA LUNYIRI TEKANISA ambao ni
wakazi wa Mtaa wa Kivukoni Kata ya Nyankumbu wamesema kuwa walimuona mtoto huyo
akielea kwenye mtaro ndipo walipochukua jukumu la kumsaidia kumtoa na
walipomtoa walimkuta amekwisha kufariki.
Ikumbukwe kuwa mamlaka
ya hali ya hewa hivi karibuni imetaja mikoa ambayo itapata mvua kwa wingi
ikiwemo na Mkoa wa Geita na kuwataka wananchi ambao wanaishi kwenye maeneo ya
mabonde kuchukua taadhari mapema kwani mvua hizo zitaendelea hadi mwezi wa
tano.
|
No comments:
Post a Comment