Mtuhumiwa Bw. Saayai Petro ambaye anashitakiwa
kwa kumuoa Binti wa miaka 16 akiwa amekamatwa
|
Mzee Kashirima
Kashimba ambaye ni Baba wa Binti huyo akiwa amekamatwa baada ya kuwakimbia
askari.
Kamanda wa Polisi Mkoani Geita, Mponjoli
Mwabulambo akielezea hatua za kushikiliwa mzazi wa Binti huyo na dada yake na
mwanaume ambaye alikuwa amemuoa.
|
Ikiwa serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasisitiza wanafunzi kupelekwa
shule na kupatiwa Elimu Bure Hali imekuwa ni Tofauti kwa Binti
mwenye umri wa miaka 16 ambaye anatoka Kata ya Kanyara Wilayani
Geita amejikuta akilazimishwa kuozeshwa na mzazi wake wa kiume baada ya
kumaliza darasa la saba na kufaulu kuendelea na masomo ya kidato
cha kwanza kwenye shule ya sekondari ya Kasamwa.
Binti huyo Alifaulu
mwaka 2017 kuingia kidato cha kwanza mwaka 2018 katika shule ya sekondari
Kasamwa lakini hakuwahi kuhudhuria masomo hata siku moja.
Baba mzazi
aliyejulikana kwa jina la Kashirimu Mashimba amepokea posa ya Ng’ombe watano
kutoka kwa Saayai Petro aliyetaka kumuoa binti mwenye umri wa miaka 16.
Kaimu afisa mtendaji
wa Kata ya Kanyara Bw,Augustino Kazanza amesema kuwa walibaini kuwa binti huyo
amehozeshwa kutokana na kupata taarifa kwa wananchi wenye mapenzi mema.
Mkurugenzi wa
halmashauri ya Mji Mhanidisi Modest Aporinaly amesema kuwa bado kuna changamoto
ambazo zimeendelea kujitokeza kwa watoto wa kike kupata mimba wakiwa shuleni
kutokana na baadhi ya watu kuendelea kuendekeza mali na kuacha kuwapa Elimu
wasichana.
Mkuu wa wilaya ya
Geita,Mwl Herman Kapufi amelaani kitendo hicho na kuwataka wananchi kuwa mstari
wa mbele kutoa taarifa dhidi ya watu ambao wanawahozesha wanafunzi
Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Geita Mponjoli Mwabulambo amesema hadi sasa wanawashikilia watu watatu
ambao ni Dada,Baba pamoja na kijana ambaye ndiye muoaji
Ikumbukwe tu kuwa Mkoa
wa Geita katika takwimu za wanafunzi watoro inashika nafasi ya Pili kwa
Skondari asilimia 8.1 na msingi asilimia 3.1
No comments:
Post a Comment