Baadhi ya Wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) katika kikao chao na Mkuu huyo wa Mkoa kilichofanyika jana Mjini Bariadi.
|
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na Wafanyabiashara wa Mkoa huo katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi.
|
Baadhi ya Wafanyabiashara wa Mkoa wa Simiyu, wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka(hayupo pichani) katika kikao chao na Mkuu huyo wa Mkoa kilichofanyika jana Mjini Bariadi.
|
Kauli hiyo ilitolewa
na Wafanyabiashara hao katika kikao chao na Mkuu wa Mkoa kilichofanyika
jana Mjini Bariadi, ambacho kilifanyika kwa lengo la kuzungumzia fursa za
biashara na uwekezaji zilizopo mkoani humo, changamoto zinazowakabili na
utatuzi wake.
Awali akifungua kikao
hicho, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema Serikali mkoani humo
imekusudia kuwa na shule kubwa itakayoweza kuchukua wanafunzi 1000 ambayo
itakayopatikana kwa kujenga upya shule ya Sekondari Simiyu (Kidato cha kwanza
hadi cha Nne), ambapo aliahidi kuwa ofisi yake itatoa fedha kiasi na akawaomba
wafanyabiasha wazawa kuchangia Ujenzi wa shule hiyo kwa ajili ya maendeleo ya
Mkoa.
Amesema pamoja
na kujenga upya Shule ya Sekondari Simiyu, katika shule hiyo kutajengwa mabweni
kwa ajili ya wanafunzi wa kike ili wanafunzi wote wa kike wasome wakiwa
wanafunzi wa bweni(boarding).
Ameongeza kuwa shule
hiyo itakuwa ikichukua wanafunzi watakaofanya vizuri kutoka katika wilaya
nyingine ili waandaliwe vema na kuimarisha shule za Kidato cha Tano na Sita na
kuwa katika uwezo wa kushindana na wenzao kutoka mikoa mingine.
Aidha, amesema mara
baada ya kukamilisha kuimarisha Shule ya Sekondari ya Simiyu Mkoa huo
umedhamiria kuwa na Shule ya Sekondari ya Wasichana Simiyu na Shule ya
Sekondari ya Wavulana Simiyu, ambazo zitapatikana kwa Kujenga Upya
au kubadili zilizopo kwa kibali maalumu cha Wizara yenye dhamana na
Elimu, ili kuwa na shule mbili za mkoa moja ya wasichana na nyingine ya
wavulana.
"Hatuwezi kuwa
Makao Makuu ya Mkoa ambayo elimu yote inaishia Shule za Kata, ni lazima
tutengeneze shule ambayo watoto wetu wakifanya vizuri katika wilaya zetu
wanakuja kusoma hapa; hatuwaweza kushindana na kufanya mambo yote mazuri
tuliyojadili hapa ya viwanda na mengine kama hatutaelimisha watu wetu"
alisema.
Mwenyekiti wa Chama
cha Wafanyabiashara Mkoa wa Simiyu Bw. Njalu Silanga amesema Wafanyabiashara
wako tayari kuunga mkono juhudi za Serikali katika ujenzi wa Shule ya Mkoa
jambo ambalo litakuwa mwendelezo wa kile kilichowahi kufanyika miaka iliyopita
ambapo wafanyabiashara hao walijenga shule ya Sekondari Biashara na kuikabidhi
kwa Serikali.
“Sisi wana Simiyu
tunapenda maendeleo, tumewahi kukusanywa kama hivi leo tukakubaliana tukajenga
Shule ya Sekondari Biashara tukaikabidhi Serikali, pia wapo watu hapa kwenye
maeneo yao wamejenga madarasa tena ya viwango wakaikabidhi Serikali, kujenga Shule
ya Sekondari ya Mkoa inawezekana” alisema Njalu.
Wakati huo huo
wafanyabiashara hao wameahidi kuwashirikisha Wafanyabiashara wengine ambao ni
wazaliwa wa Mkoa wa Simiyu wanaofanya biashara zao katika mikoa mingine ili
washirikiane katika kufanikisha Ujenzi wa Shule ya Sekondari Mkoa wa Simiyu.
No comments:
Post a Comment