Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku Musukuma amevitaka vyombo vya dola kuwashughulia watu wanaodaiwa kuwa wakorofi hasa wanasiasa kwa kuwaweka ndani ili kurekebisha tabia zao.
Msukuma alitoa wito
huo Bungeni mjini Dodoma wakati akichangia hoja katika Wizara ya Katiba na
Sheria.
“Sisi kama wabunge
tunaotunga sheria tuviachie vyombo vifanye kazi yake, wanaosema kuna watu
wamepotea hata watu wa CCM wamepotea wengi tu, wamechinjwa Kibiti wengi tu na
hatukupiga kelele tumeviachia vyombo vinalishughulikia.
"Hata mimi
nilifanya kosa na niliwekwa ndani. Hawa wakorofi wakifanya makosa wawekwe
magereza, unamuona Lema sasa hivi kidogo amekuwa binadamu,” alisema.
Aidha, Msukuma
alimuomba Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi kupeleka bungeni
muswada wa kubadilisha sheria ili makosa yasiyo stahili mtuhumiwa kufungwa
apewe adhabu ndogo ili kuondoa msongamano wa wafungwa magerezani.
No comments:
Post a Comment