Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa Nje ya vibanda vyao baada ya kufungwa na Halmashauri ya Mji wa Geita. |
Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa wamekaa wakitafakari hatua ya kufungiwa kwa vibanda vyao hali iliyowapelekea kushindwa kuendelea na Biashara. |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita,Leornad Bugomola akizungumza na wafanyabiashara baada ya kufika na kujionea hali hiyo. |
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinaly akizungumza juu ya hatua ambayo imechukuliwa ya kuvifungia vibanda ambavyo avijalipa kodi ya elfu therasini. |
Mwanasheria wa Halmashauri hiyo Bashiri Mhoja akizungumzia kifungu ambacho kinamhurusu mkurugenzi kuvifungia vibanda vya wafanyabiashara hao kutokana na kukiuka makubaliano. |
Zaidi ya vibanda
Hamsini (50) vya Wafanyabiashara kwenye Stendi kuu ya Mkoa wa Geita
vimefungwa kwa madai ya kukaidi agizo la kulipa kodi iliyo pangwa na
Halmashauri ya Mji wa huo.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti baadhi ya wafanyabiashara hao Bi. Mwajuma
Hassani na Bw. Sadick Mbido wameilalamikia Halmashauri ya mji wa
Geita kwa kitendo cha kukiuka makubaliano ya mkataba kwani kwasasa walikuwa
wanalipa kodi ya Tsh. elfu kumi (10,000) kwa mwezi ambapo ilikuwa ni ya
mkataba unaoisha mwaka 2020 na kwamba ni jambo lililowashangaza
kutokana na kulazimishwa kulipia kiasi cha Tsh. Elfu thelathini (30,000).
Hata hivyo
Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Stendi hiyo, Bw. Hamis Ayaki amesema
kuwa kitendo ambacho kimefanyika ni ukiukwaji wa makubaliano na kipo kinyume na
makubaliano na kwamba ameelezea namna ambavyo mkataba ulikuwa ukisema.
Kwa upande wa Katibu
wa Wafanyabiashara Bw. Isack Shoo ameiomba Serikali kuwasaidia kutokana na wao
kuendelea kulipia mapato ya Serikali na kwamba wana familia ambazo
zinawategemea hivyo kufanya hivyo ni sawa na kuwaonea na kuwanyima haki zao za
msingi.
Akizungumza na
Wafanyabiashara hao baada ya kufika na kujionea kufungwa kwa Shughuli zao Mwenyekiti
wa Halmashauri ya mji wa Geita, Bw. Leornad Bugomola amewataka kuwa watulivu na
kwamba suala lao litashughulikiwa kwa wakati na watarudi kuendelea na shughuli
zao.
“Ndugu zangu kwanza
niwashukuru maana mmekuwa watulivu mmenipigia simu nimekuja na ndio tunataka
namna hii sio kujichukulia hatua mkononi mimi nawaomba muwe watulivu
ikiwezekana niondoke na viongozi wenu hili tufuatilie suala hili na
likikamilika watawaletea majibu” Alisema Bugomola.
Kutokana na malalamiko
hayo Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Geita,
Mhandisi Modest Aporinaly alisema wameshakaa na wamiliki wa Vibanda na
wakaelewana kuwa watalipa Tsh. Elfu thelathini hivyo kitendo ambacho
wanakiona ni ukiukwaji wa makubaliano baina ya wamiliki wa Vibanda na
Wapangaji.
Mwanasheria wa
Halmashauri hiyo Bashiri Mhoja amesema kuwa ndani ya mkataba kipengele
namba tatu (3) kinamruhusu Mkurugenzi kufanya mabadiliko baada ya
kipindi cha miaka mitatu kutokana na mfumuko wa Bei.
No comments:
Post a Comment