Vijana therasini ambao ni Raia wa nchi ya Burundi wakiwa wameshikiliwa na Idara ya uhamiaji Mkoani Geita Kabla ya kufikishwa mahakamani. |
Naibu kamishina wa idara ya uhamiaji Mkoani Geita, Wilfred Marwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake. |
Idara ya uhamiaji Mkoani Geita imewakamata Raia wa Burundi Therasini (30) ambao wanaishi na kufanya kazi Nchini kinyume cha sheria na wengine wakikamatwa kwenye zoezi la kujiandikisha vitambulisho vya Taifa ambalo linaendelea Mkoani humo.
Akizungumza na
waandishi wa habari kwenye ofisi za uhamiaji Mkoani humo, Naibu kamishina wa
idara ya uhamiaji Mkoani Geita, Wilfred Marwa amesema kati ya hao
Raia kumi na nane ( 18) wapo nchini
kinyume na sheria na wanafanya kazi mbalimbali za kujiingizia kipato na
wengine kumi na mbili (12) walikuwa kwenye zoezi la kujiandikisha
vitambulisho vya Taifa jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Naibu kamishina Marwa
ametaja kazi ambazo wamekuwa wakizifanya Raia hao wa kigeni kuwa ni kazi za
kilimo na ufugaji.
“Mara nyingi watu hawa
wanajishughulisha sanaa na kazi za ufugaji wa Ng’ombe na kilimo cha
Mananasi pamba na
mpunga kwenye maeneo ya vijijini” Alisema Marwa.
Aidha kwa upande wake
moja kati ya Raia wa Burundi aliyekamatwa na idara ya uhamiaji Bw,Kajoro
Richard alisema sababu ambazo zimekuwa zikisababisha kuingia nchini ni kutokana
na ugumu wa maisha nchini mwao na kukosekana kwa ajira.
“Mimi Kweli nilikuja
hapa Tanzania nikitokea nchini kwetu Burundi kwa sababu ya kuja kutafuta maisha
kwetu ajira ni ngumu sanaa ila naomba wanisamehe nipo tayari kurudi nchini
kwetu”Alisema Kajoro.
Naibu kamishina
Wilfred Marwa amesema zoezi hilo ni endelevu na kwamba amewataka raia wa kigeni
kufuata utaratibu kwa kufuata vibari vya kukaa nchini kwa njia ya halali huku
akiwataka watanzania ambao wanaishi na Raia hao kuachana na tabia hiyo na
kwamba watakamatwa watafungwa kifungo cha miaka 20 au faini ya milioni
ishirini 20.
No comments:
Post a Comment