Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa mara
nyingine umefanya zoezi la kuwasaidia wakazi wa Geita wenye matatizo ya mdomo
sungura na wenye uvimbe kwenda kufanyiwa upasuaji jijini mwanza katika
Hospitali ya Sekoture ikiwa ni muendelezo wa kusaidia jamii inayowazunguka
katika kuwapa huduma mbalimbali za kiafya wananchi
Zoezi la kuwasaidia wenye midomo sungura hufanyika kwa mwaka mara mbili ambapo kwa mwezi huu wa nne jumla ya watu wazima
pamoja na watoto 25 wamepata nafasi ya kwenda kutibiwa.
Akiwaaga baadhi ya wagonjwa ambao wanatarajia
kwenda kufanyiwa upasuaji kwenye Hospitali ya Sekoture ililiyopo jijini Mwanza Mkuu wa Wilaya ya Geita
Mwl. Herman Kapufi amewataka watu wengine kuwa na upendo na umoja ikiwa ni
pamoja na kutoa taarifa kwa mtu ambaye anatatizo hilo pindi anapoitajika.
Ni zaidi ya watu laki saba wamekwisha kutibiwa
tangu zoezi lianze mwaka 2014 .
No comments:
Post a Comment