Tuesday 3 April 2018

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE ASHINDWA KUZINDUA MIRADI KUTOKANA NA TAARIFA ZA FEDHA KUTOFAUTIANA GEITA





Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Charles Kabeho ameshindwa kuzindua mradi wa maji kwenye kijiji cha Kaboha Kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale kutokana na taarifa ya  gharama za ujenzi kutofautiana na  ya Mkoani. 

Kiongozi wa Mbio za mwenge wa uhuru Charles Kabeho ameshangazwa na taarifa hizo kutofautiana kutokana na ya Mkoa wa Geita kuonesha jumla ya sh,milioni ishirini na tano na laki tano na fedha kutoka serikali kuu ni milioni ishirini na nne na laki nane na sitini na kwamba  wilaya ya Nyang’hwale fedha  zilizotoka  serikali kuu ni milioni 14 laki 2 na 15 hali ambayo ilimpelekea kuwa na wasiwasi juu ya mradi huo.

No comments:

Post a Comment