Serikali imezindua utoaji chanjo ya
kudhibiti saratani ya shingo ya kizazi kwa watoto wa kike wa umri kati ya miaka
TISA (9) na miaka 14.
Akizungumza
kwenye shughuli hiyo Makamu wa rais kwa upande wake amesema ni jambo jema kwa
Taifa kuwa na wananchi wenye afya na kuwalinda watoto katika magonjwa
hatarishi.
Aidha Makamu wa Rais amewaagiza Waganga Wakuu
na Wilaya kuandaa kambi za wazi angalau mara tatu kwa mwaka ili kutoa fursa kwa
wanawake wengi zaidi kupima saratani ya matiti nay a mlango wa kizazi.
Makamu wa Rais amesema Utoaji wa Chanjo dhidi
ya Saratani ya mlango wa kizazi pamoja na uchunguzi wa awali kwa pamoja
vitasaidia kuwakinga mabinti na kubaini mapema ugonjwa wa saratani kwa wanawake
na hivyo kuepusha maumivu makali ama vifo vinavyoweza kuzailika
“ Tunatakiwa hadi Desemba, 2018 tuwe
tumewafikia wanawake milioni tatu. Hii itawezekana endapo kila mmoja wetu
ataweka kipaumbele katika kufikia lengo hilo.” Amesisitiza Makamu wa
Rais.
Makamu wa Rais amesema kuwa Serikali itatoa
chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi bila malipo yoyote katika vituo
vinavyotoa huduma za chanjo vya Serikali, Mashirika ya Dini na Taasisi Binafsi.
No comments:
Post a Comment