Mratibu msaidizi wa afya ya uzazi Mkoani Geita,Bi Mbeleje Donald akitoa maelekezo ya namna ambavyo watoa huduma wanatakiwa kuzingatia wakati wa zoezi la Chanjo ya mlango wa uzazi.
Mkoa wa Geita
unatarajia kuanza zoezi la chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi
kwa Wasichana wenye Umri wa miaka kumi na nne(14) lengo likiwa ni kuwakinga na maambukizi
ya virusi vya Human Papilloma.
Saratani ya Mlango wa
kizazi imekuwa ikiongezeka kila mwaka kwa nchi na takribani watu elfu
hamsini wamekuwa wakiongezeka na kusababisha vifo vya wakina mama wengi
pamojana na mabinti.
Akizungumza na wadau
wa sekta ya afya Mkoani hapa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel
ametaja sababu ambazo zimeendelea kusababisha Saratani ya mlango wa
kizazi ni pamoja na kujamiiana kwenye umri mdogo, kuwa na wapenzi
wengi, ndoa za mitaara pamoja na uvutaji wa sigara.
“Ndugu washiriki
kuna dalili ambazo zinaweza kusababisha ugonjwa wa saratani Kuto kwa damu bila
mpangilio au kutokwa damu baada ya kujamiana Maumivu ya mgongo, miguu na au
kiuno Kuchoka, kupungua uzito, kupungikiwa hamu ya kula Kutokwa uchafu uchafu
kwenye uke wa majimaji, uliopauka wa rangi kahawia au wenye damu Kuvimba mguu
mmoja”
Alisema Robert.
Kwa upande wake
Mratibu msaidizi wa Afya ya uzazi Mkoani humo,Bi Mbeleje Dornad alisema kwa
hapa nchini takribani wanawake laki nne na sitini na tisa elfu wamegundulika na
maambukizi ya saratani ya mlango wa kizazi.
“Inakadiriwa kuwa kila mwaka kati
ya wanawake 466,000 wanathibitika kuwa na saratani ya mlango wa kizazi,
na wengi wao wako katika nchi zinazoendelea” Alisema Bi,Mbeleje.
Kaimu Mganga mganga
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Joseph Odero amewataka wazazi pamoja na walenzi kutoa
ushirikiano pindi zoezi hilo litakapo anza tarehe 23 mwezi huu wa aprili hikiwa
ni pamoja na kuwaruhusu mabinti wenye umri wa miaka 14 kufanyiwa chanjo hiyo.
Takwimu kutoka
hospitali ya Occean Road inaonyesha kwamba, Saratani ya Mlango wa Kizai
inachangia kwa asimilia 36 ya saratani zote, Asilimia 70 ya wagonjwa wa
saratani ya mlango wa kizazi wanajitokeza katika hatua ambayo tayari saratani
imesha samba maeneo mengine mwilini.
|
No comments:
Post a Comment