Mamlaka ya hali ya hewa iliyopo chini ya
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania imewatahadharisha
wananchi kuwepo kwa vipindi vya mvua kubwa katika maeneo yote ya pwani kuanzia
leo usiku mpaka Aprili 16 mwaka huu.
Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na mamlaka
hiyo jioni ya leo (Ijumaa) na kudai kutakuwepo vipindi vya mvua kubwa inayozidi
milimita 50 katika saa 24 ambavyo vinatarajiwa katika maeneo ya mkoa wa Tanga,
Dar es Salaam, Morogoro, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Aidha, TMA imewashauri wakazi wa maeneo
yaliyotajwa kuchukua tahadhari stahiki na kuendelea kufuatilia taarifa pamoja
na tahadhari zinazotolewa.
No comments:
Post a Comment