Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza katika Mkutano wa Tano wa Taasisi za Fedha
za Kiislamu Afrika uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya
Kilimanjaro Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam. Masauni aliwataka Watanzania
kuweka Fedha zao katika Benki za Kiislamu zilizopo nchini ambazo hazina riba
ili ziwasaidie katika mafanikio mbalimbali. Pia Masauni aliipongeza Taasisi
hiyo kwa kuwekeza nchini. Kulia ni Kamishna wa Bima katika Mamlaka ya Usimamizi
wa Shughuli za Bima nchini (TIRA), Dk. Baghayo Saqware, na katikati ni Naibu
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bernard Kibesse. Picha na Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni (kulia), akimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi za Fedha za
Kiislamu Afrika, Muhammad Mughal alipokua anaishukuru Serikali ya Tanzania kwa
ushirikiano wake kwa Taasisi yake. Hayo alizungumza katika Mkutano wa Tano wa
Taasisi hiyo uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Kilimanjaro
Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam. Masauni aliwataka Watanzania kuweka Fedha
zao katika Benki za Kiislamu zilizopo nchini ambazo hazina riba ili ziwasaidie
kupata mafanikio zaidi. Wapili kulia ni Kamishna wa Bima katika Mamlaka ya
Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA), Dk. Baghayo Saqware, na watatu
kulia ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bernard Kibesse. Picha na
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza katika Mkutano wa Tano wa Taasisi za Fedha
za Kiislamu Afrika uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya
Kilimanjaro Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam. Masauni aliwataka Watanzania
kuweka Fedha zao katika Benki za Kiislamu zilizopo nchini ambazo hazina riba
ili ziwasaidie katika mafanikio mbalimbali. Pia Masauni aliipongeza Taasisi
hiyo kwa kuwekeza nchini. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akimpa zawadi Kamishna wa
Bima katika Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima nchini (TIRA), Dk. Baghayo
Saqware. Kushoto ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Bernard Kibesse,
kulia ni Balozi wa Nigeria, nchini, Dk. Sahab Isa Ga, na wapili kulia ni Afisa
Mtendaji Mkuu wa Taasisi za Fedha za Kiislamu Afrika, Muhammad Mughal. Mkutano
wa Tano wa Taasisi hiyo umefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya
Kilimanjaro Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam, ambapo Masauni alikua mgeni
rasmi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wanne kutoka kulia mstari wa mbele),
akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Taasisi za Fedha za Kiislamu Afrika
pamoja na washiriki wa Mkutano wa Tano wa Taasisi hiyo uliofanyika katika Ukumbi
wa Mikutano wa Hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam.
Masauni ambaye alikua mgeni rasmi katika mkutano huo, aliwataka Watanzania
kuweka Fedha zao katika Benki za Kiislamu zilizopo nchini ambazo hazina riba
ili ziwasaidie kupata mafanikio zaidi. Pia Masauni aliipongeza Taasisi hiyo kwa
kuwekeza nchini. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment