Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama onyesho
la halaiki, wakati alipokagua maandalizi ya sherehe za miaka 54 ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar, kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 24, 2018.
Kutoka kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera na Uratibu) Profesa
Faustine Kamuzola, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge, Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ,
Jenista Mhagama, Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dr
Florens Turuka, naMkuu wa Majeshi ya Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo
Askari wa Jeshi la Magereza, wakionesha zoezi la
kupambana na adui mbele Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, wakati alipokagua
maandalizi ya sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwenye
uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 24, 2018
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiwapungia
wananchi, wakati alipokagua maandalizi ya sherehe za miaka 54 ya Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar, katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 24, 2018
Waziri mkuu Kassim
Majaliwa amesema ameridhishwa na maandalizi ya sherehe za miaka 54 ya Muungano
wa Tanganyika na Zanzibar yanayoendelea katika Uwanja wa Jamuhuri mjini Dodoma.
Ameyasema hayo leo
(Jumanne, Aprili 24, 2018) mara baada ya kukagua maandalizi hayo yanayofanyika
kwenye Uwanja wa Jamuhuri mjini Dodoma, ambapo amesema maandalizi yanaendelea
vizuri.
Waziri Mkuu amejionea
maonesho mbalimbali yakiwemo ya kikundi cha halaiki ambacho kinaundwa na
wanafunzi 2,000 kutoka Manispaa ya Dodoma pamoja na maonyesho ya kujihami na
maadui yaliyooneshwa na Jeshi la Magereza.
“Nimeridhika na kazi
ambayo mmeifanya, nawaruhusu muendelee kushirikiana katika kukamilisha maeneo
ambayo yamesalia na kuanzia kesho tujiandae kuwapokea wageni kutoka maeneo
mbalimbali.”
Alhamisi Aprili 26, 2018
Watanzania wanatarajia kuadhimisha miaka 54 ya Muungano tangu Tanganyika
ilipoungana na Zanzibar, chini ya waasisi wake Hayati Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume.
No comments:
Post a Comment