Moja kati ya mwananchi (hayupo kwenye picha)
akipima maralia kwenye viwanja vya Nyankumbu Mjini Geita.
|
Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel
akiwakabidhi baadhi ya akina mama vyandarua vyenye dawa ya kuua mbu
vinavyotolewa bure na serikali kwa wananchi.
Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel
akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
|
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji
wa Geita akiwasilisha salamu zake kwenye maadhimisho hayo.
|
Ikiwa ni siku mbili
zimepita tangu kuadhimisha siku ya Malaria Mkoa wa
Geita maambukizi ya ugonjwa huo yameshuka kutoka asilimia
38.1 mwaka 2015/17 hadi asilimia 17 mwaka 2017/18 kwa mjibu wa takwimu za
Tanzania Demographic and Health Survey (TDHS).
Akizungumza na
wananchi kwenye viwanja vya Nyankumbu Mjini Geita wakati wa utoaji wa
elimu juu ya kujikinga na maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria Mkuu
wa
Mkoa wa Geita,
Mhandisi Robert Gabriel amesema mafanikio hayo ni matokeo ya kazi
nzuri ya serikali ya awamu ya tano ambayo imedhamiria kuondoa vifo
vinavyotokana na Malaria ambapo takwimu zinaonyesha kwamba wastani wa mtu mmoja
hupoteza maisha kila baada ya dakika moja kutokana na ugonjwa huo unaoambukizwa
na mbu jike aina ya “Anopheles”.
Ameongeza kuwa serikali
kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya inaendelea na mapambano dhidi ya
Malaria ambapo mwaka jana ilitoa lita 8,380 za dawa ya viua dudu katika mazalia
ya mbu pamoja na kugawa bure vyandarua vyenye dawa kwa wananchi.
Mganga Mkuu mkoani
Geita, Dr.Japhet Simeo Amebainisha kwamba mkoa wa Geita unasumbuliwa na
maambukizi ya Malaria kutokana na sababu za kimazingira ambapo kuna nyuzi joto
18 hadi 32 linalochochea uendelevu wa mbu hivyo ni vyema wananchi wakahakikisha
wanatunza vyema mazingira yao ikiwemo kufyeka nyasi na kufukia madimbwi ili
kuangamiza mazalia ya mbu.
Wananchi na wanafunzi
mkoani Geita waliitikia vyema zoezi la upimaji Malaria na utoaji bure dawa kwa
waliobainika kuwa na ugonjwa huo .
No comments:
Post a Comment