Rais John Magufuli
jana alimmwagia sifa Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda kwa kumwelezea ni
kiongozi mkimya na asiyependa kuzungumza ovyo ovyo.
Rais Magufuli alisema
Pinda, maarufu kama Mtoto wa Mkulima, ni kiongozi anayefaa kuigwa na viongozi
wengine, na kwamba hata yeye siku akistaafu atamfuata ili kujifunza.
Aliyasema hayo jana
mjini Dodoma wakati akifungua Tawi la Benki ya NMB la Kambarage na Jengo la
Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF).
“Mzee Pinda anaishi
maisha ya kawaida sana, hapigi kelele, hazungumzi chochote, Mzee Pinda ‘you are
too special’ (wewe ni mtu wa kipeke),” alisema Rais Magufuli.
“Watu watakukumbuka
(Pinda) kwa ukarimu wako, wewe ni mtu wa kawaida sana. Sasa hivi hatujui
thamani yako lakini ipo siku tutaijua.
“Ndiyo maana bado
unaonekana kijana, hujipi ‘pressure’ (hofu), unaamini kile unachofanya, na mimi
nikistaafu nitakuja kuchukua ‘course’ (mafunzo) kwako.”
Sifa kwa Pinda
zinakuja miezi saba tangu alipokosoa viongozi wastaafu wa "maeneo
mengine" wanaosemasema kila wakati kuhusu uendeshaji wa serikali.
Akizungumza jijini Dar
es Salaam Septemba 11, mwaka jana Rais Magufuli alitoa mfano wa majaji wastaafu
ambao alisema ni tofauti na wastaafu wengine na kwamba huenda kujua sheria
ndiko kunakowasaidia kutokuwa waropokaji.
Rais Magufuli alisema
hayo wakati wa kumuapisha Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma.
“Nawashuruku majaji
wakuu wastaafu, Barnabas Samatta na Augustino Ramadhani, walifanya kazi kubwa ya
kujenga misingi ya mahakama nchini," alisema.
“Bahati nzuri majaji
hawa ni waadilifu sana huwezi kumsikia Jaji (Mkuu mstaafu Othman) Chande,
(Barnabas) Samatta, Augustino (Ramadhani), (Damian) Lubuva au majaji walioko
hapa... ukiangalia wastaafu wa maeneo mengine hawachoki kusema,
wanawashwawashwa.
“Ndiyo maana
nawapongeza sana mahakama...Ni safi mno, nina uhakika wanapotaka kutoa ‘advice’
(ushauri) yoyote (wowote) lazima wanakushirikisha (Jaji Mkuu); ndiyo faida ya
kujua sheria.
“Sisi wengine huku ambao
hatujajua sheria mahali popote, chochote unaweza ukazungumza.”
No comments:
Post a Comment