Waziri
mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa Kassim akijibu Swali
lililoulizwa na Mbunge Viti Maalum Upendo peneza, Bungeni Mjini Dodoma
Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa, ameshauri Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Upendo Peneza, kukaa na
Waziri wa Fedha na Mipango na yule wa Tamisemi, kushauriana njia bora ya
kuhakikisha taulo za kike zinapatikana kwa bei nafuu ambazo wanafunzi
walioshindwa kwenda shule wakati wa hedhi watazimudu.
Kauli hiyo ya Majaliwa
imekuja baada ya Pendeza kutaka kauli ya Serikali juu ya kondoa kodi kwenye
taulo hizo, akisema baadhi ya wanafunzi kutoka kaya masikini wamekuwa
wakishindwa kuhudhuria mawasomo wawapo kwenye hedhi kwa sababu ya kushindwa
kumudu taulo hizo za kujisitiri.
“Kwa kuwa lengo la
serikali ni kuhakikisha inaondoa vikwazo vyote kwenye elimu, na Waziri wa
Tamisemi alishaelekeza zile Sh 10,000 na Sh 20,000 zinazopelekwa kama ruzuku
kwa shule za msingi na sekondari zitumike kununua taulo hizo, lakini
ikizingatia fedha hizo ni kidogo, kwanini sasa Serikali kwenye sheria ya fedha
inayokuja isiondoe kodi kwenye taulo hizi ili wanafunzi kutoka kaya masikini
waweze kuzimudu,” aliuliza Peneza wakati wa maswali ya papo kwa papo kwa Waziri
Mkuu.
Akijibu swali hilo,
Majaliwa alisema “Serikali ina utaratibu wake wa kuondoa kodi kwenye bidhaa
zinazoleta tija ikiwamo uliyoisema mheshimiwa Mbunge, kwa kuwa serikali imeanza
kutoa fedha kama ulivoeleza, Wizara ya fedha na Waziri (TAMISEMI) wataona
namna mtakavyokaa kuona jinsi ya kupunguza bei kwenye vifaa ulivyoeleza.”
No comments:
Post a Comment